Joshua justine
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 792
- 1,015
Huku ndiko taifa tunaelekea, uwezo wa kuhoji maswala muhimu unaongezeka na watu wanazidi kuelimika kuhusu maswala ya sayansi ya uraia, na hizi ndizo athari chanya za matumizi ya mitandao kijamii.
=========
Wananchi wamekuwa wakifatilia ubadhirifu huu kwa kupiga simu na kupitia mitandao ya kijamii wakihoji juu ya ubadhirifu wa Tsh Mil 327 na maamuzi yaliyofanywa na Baraza la Madiwani. Serikali imeamua kutoa ufafanuzi ili mjadala huo ufungwe na wananchi waendelee na shughuli zao.
Ufafanuzi huo utahusisha hatua za kinidhamu zilizochukuliwa kwa watumishi watatu waliyohusika katika ubadhirifu huu wa Tsh. 327;
1) Sababu ya kutoa taarifa hii kwa umma
Imeonekana ni hitaji la wananchi kutaka kujua kulikoni, kwasababu siyo taarifa ya siri tena.
2) Taarifa ya uamuzi wa kuwarejesha kazini watumishi waliohusika na ubadhirifu huu kuwa ya siri sababu ulijadiliwa kwenye kamati ya Baraza la Madiwani
Kilichokuwa siri ni majadiliano ya ndani ya Baraza la Madiwani wakati baraza hili lilipokuwa kamati ya nidhamu, baada ya kamati kumaliza mchakato wake na kurudi kuwa Baraza la Madiwani, walitangaza maamuzi wa kamati iliyokuwa inaendesha mchakato wake kwa usiri mkubwa.
Kufuatia mjadala uliyokuwa unaendelea mitandaoni na kwamba Madiwani wametoa adhabu wa kuwarejesha kazini na kuwakata 15% ya msharaha kwa kila mmoja kwa muda wa miezi 36, ukweli ni kwamba upotevu huo ulifanyika katika kipindi cha Jan 2019, baada ya uchunguzi kuanzia jan 2019 - Dec 2021 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa wa Bukoba alipewa taarifa ya uchunguzi huo.
Mkurugenzi alitimiza wajibu wake kwa kuunda kamati ya uchunguzi ili kumuwezesha kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watuhumiwa hao kabla ya kutiwa hatiani katika mchakato wa kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.
Katika uchunguzi wa kamati iliyoundwa na Mkurugenzi, watumishi watuhumiwa watatu walitiwa hatiani na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yao. Adhabu iliyotolewa na Madiwani ni kuwakata 15% ya mishahara yao kwa muda wa miezi 36 (miaka mitatu).
Adhabu hiyo ni miongoni mwa adhabu tatu zinazokubalika kutolewa kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma, mtumishi anaweza kupewa adhabu moja wapo kati ya tatu kutokana na makosa waliyotenda;
Diwani wa Halmashuri ya Manispaa Bukoba chini ya Mstahiki Meya Godson Gipson waliamua kutoa adhabu ya kuwakata 15% ya mishahara yao kwa miaka 3. Kisheria inakubalika adhabu hiyo kwani wana haki ya kuchagua aina ya adhabu ya kuwapatia.
Hata hivyo adhabu waliyotoa inaonekana ni ndogo kulingana na kosa walilofanya na ndiyo maana umma umetaharuki. Adhabu hiyo ni ndogo kwasababu ngazi ya mishahara yao ni kwamba wawili wana TGSE mwingine ana TGSB, hivyo wakikatwa kwa miaka mitatu wataweza kuirejeshea serikali makadirio ya kiasi kisichozidi 13,500,000 kila mmoja kati ya milioni 327 zilizofanyiwa ubadhirifu.
Mbali na hatua hizo za kinidhamu, TAKUKURU mkoa wa Kagera wanaendela na uchunguzi na watakapokamilisha watawafikisha mahakani kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayowakabali. Vilevile baadhi ya mali za watuhumiwa zinashikiliwa na TAKUKURU Kagera wanapoendelea na uchunguzi wao kwa mujibu wa sheria.
Nawaomba na kuwasihi wananchi wote wa Bukoba kutulia wakati TAKUKURU wanaendelea na uchunguzi wao unaohusisha nyaraka nyingi, pindi wakatapomaliza uchunguzi wao watachukua hatua stahiki.
Mtumishi anapofanya ubadhirifu ni suala lake binasfi, hajatumwa na kiongozi yeyote wala CCM, ndiyo maana hata sisi viongozi ambao baadhi tunatoka chama kinachounda serikali, tunasimama kukemea na kuchukua hatua madhubuti dhidi ya vitendo hivyo.

- Mtumishi anaweza kufukuzwa kazi.
- Kushushwa cheo na kukatwa mshahara.
- Kukatwa 15% kwa mwezi kwa muda miaka mitatu mfululizo (Miezi 36).