1. Taka zenye kemikali eneo la Soko la Samaki na Kamanga Beach
Sisi wakazi wa pembezoni mwa Ziwa Victoria tumekuwa tukishuhudia mambo mengi ambayo ni hatarishi kwa usalama wa ziwa lenyewe na hata Wananchi mbalimbali, hiyo ni kutokana na utupaji wa taka ngumu na zenye Kemikali unaendelea pembezoni mwa maeneo ya Ziwa hilo.
Kuna magari ya makampuni huwa yanakuja na kutupa chupa ama baadhi ya vitu mbalimbali pembezoni mwa Ziwa Victoria.
2. Uvuvi eneo la MIHAMA-KITANGIRI na MKUYUNI SOKONI
Baadhi ya maeneo kuna wavuvi wanaendelea na tabia ya kuvua kwa njia ya haramu kwa kutumia vifaa visivyo salama hali ambayo inaathiri samaki na mazalia yake.
4. Maji machafu ni mifereji ipo sehemu mbalimbali mjini inamwaga maji Ziwa Victoria
Baadhi ya Wananchi wameeleza Kutokana na Jografia ya Mkoa wa Mwanza kuna maeneo bado korofi ambayo hutiririshwa maji machafu hasa wakati wa mvua, wakaazi wa maeneo ya milimani hufungulia vyoo na hutiririshwa maji machafu.
Wameeleza pia kuna maeneo bado kuna maji machafu ambayo hupita kwenye mifereji ambayo hutoka kwenye maeneo mbalimbali na humwaga maji kwenye Ziwa Victoria.
5. Kilimo katika Eneo la MIHAMA-KITANGIRI pamoja na NERA pembezoni mwa ziwa, baadhi ya Wananchi wanaofanya shughuli za kilimo wamekuwa wakifanya bila kujua taratibu mbalimbali zinazoweza kuwaongoza ili kuzuia uchafuzi na uharibifu wa ardhi na maji.
Kwa msingi huo, elimu bado inahitajika ili Wananchi waweze kufahamu namna nzuri ya kulinda Ziwa Victoria kutokana na wao kuona sawa kufanya vitu ambavyo vinaweza kuwa chanzo cha uchafuzi wa Ziwa kuwa ni hali ya kawaida.
Ushauri wangu ni kuwa kampeni za usafi wa Mazingira zinatakiwa zisiegemee siku moja ya usafi bali Wananchi wajengewe uelewa wa kufahamu faida na athari juu ya Ziwa hilo na athari za wao kuchafua mazingira.
Kumekuwa na ripoti kuwa Wananchi wanaoishi eneo la Mwaro wa Igombe mbali na unafuu wa maisha wanaoupata kuishi maeneo hayo lakini kuna changamoto za kiafya ambazo wamekuwa wakizipata zinazotokana na uchafuzi wa mazingira.
Kuna kipindi huwa wanapata changamoto ya magonjwa ya kutapika na kuhara damu, kichocho na hata kipindupindu, hiyo yote ni kutokana na maambukizi yanayohusiana na kutumia maji si safi na salama.
Uharibifu huo umekuwa ukichangia hata samaki wanaovuliwa nao kutokuwa salama sana kiafya hasa kama wanapatikana kando ya ziwa.