Wananchi wameendelea kuwa na imani kubwa na mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kuendelea kupeleka mazao yao

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Na Mwandishi wetu Mihambwe

Wananchi wameendelea kuwa na imani kubwa na mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kuendelea kupeleka mazao yao.

Wananchi mbalimbali wameonekana wakipeleka Korosho zao kwenye maghala ya vyama vya msingi ikiwa siku chache tangu msimu wa Korosho 2020/2021 kufunguliwa.

Hayo yamejitokeza kwenye ziara ya Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu wakati akitembelea Maghala mbalimbali ili kujiridhisha na utaratibu unaotumika ambapo ameshuhudia Maghala yamefunguliwa na Wakulima wanapeleka Korosho zao ghalani.

"Nimefanya ziara kutembelea Maghala mbalimbali, nimejionea imani kubwa ya Wananchi juu ya mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kupeleka Korosho zao ghalani, uwingi wa Korosho kwenye Maghala ni vitendo vinaongea vya Wakulima. Nawasihi Wananchi wazidi kuleta mapema Korosho zao ili wawahi minada ya awali ambayo mengi kihistoria yanaonekana kuwa na bei kubwa. Kadri wanavyowahi kupeleka Korosho zao ghalani ndivyo wanavyojiweka kwenye mazingira rafiki kupata bei kubwa na fedha kwa wakati." Alisema Gavana Shilatu.

Pia Wakulima wameiomba Serikali kuendelea kusimama nao pamoja ili masoko ya Korosho zao yapatikane kwa haraka na kwa bei nzuri.

"Nimepima Korosho zangu hapa ghalani, Kuna mwitikio mzuri kwa Wakulima kuleta Korosho zao na zinapatikana. Tunaomba Serikali itusimamie tupate haki zetu kwa wakati na kwa bei nzuri." Alisema Ismail Mohammed Namkoma mkazi wa kijiji cha Namunda.

Msimu wa Korosho 2020/2021 umefunguliwa tayari na Wakulima wanapeleka Korosho zao ghalani tayari kusubiri minada.
FB_IMG_1601996222379.jpeg
FB_IMG_1601996230891.jpeg
FB_IMG_1601996226117.jpeg
FB_IMG_1601996234396.jpeg
 
Option nyingine ni ipi tofauti na kupeleka huko? Isijekuwa kama ile ya kupanda ATC, yani kifupi jiwe hapendi ushindani ili aonekane mshindi.
 
Imani au hawana mbadala? Tusichanganye haya mambo mawili maana yake ni tofauti unapokuwa huna mbadala nilazima kufuata mfumo uliopo kwakupenda au kutokupenda!
 
Upumbavu huu! Yaani uzuie njia nyingine zote alafu unasema "wananchi wanafurahia"? Tutawaonesha furaha yetu tarehe 28.
 
Sasa wafanyeje wanyonge hawa ikiwa wametaitiwa kwenye kumi na nane na hawana mbadala mwingine?.
 
Back
Top Bottom