KERO Wananchi walia maombi ya Passport kukwama Uhamiaji Kibaha kwa Zaidi ya Miezi Sita: Server na Umeme zatajwa sababu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Taliban Kanye

Member
Oct 12, 2020
5
4
Tanzania, nchi ya uchumi wa kati, miongoni mwa nchi zinazoendelea kwa kasi barani Africa, yenye wananchi watiifu kwenye ulipaji kodi, inayoongozwa na serikali inayohamasisha bihashara na uwekezaji ila inakwamishwa na viongozi wachache walio kwenye sekta nyeti ikiwemo UHAMIAJI.

ZaIdi ya miezi sita wananchi waliofanya maombi ya passport katika ofisi za uhamiaji KIBAHA CBD hawajapata passport zao uku wakiambiwa ni tatizo la SERVER na UMEME ila waliofanya maombi yao makao makuu tayari walipata passport zao mapema mno. NAWASILISHA😡
 
Ni muda mrefu tangia wananchi hao kufanya maombi ya passport pale uhamiaji kibaha mjini inakaribia mwaka wananchi hawajapata passport za na hawajui wapi waende ili wapate haki zao ikiwa kama inchi yenye kupenda maendeleo ya wananchi wake na maendeleo ya taifa si vyema kuona mpaka sasa ili swala halichukuliwi hatu wala kupewa kipaumbele tunafahamu kuwa uhamiaji ni wizara nyeti na ni kubwa ambayo inachochea maendeleo ya nchi yetu wananchi wanaomba muheshimiwa mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa muwasaidie katika swala hili
 
Wananchi waomba Serikali kuchukua hatua juu ya ofisi ya uhamiaji wilayani Kibaha mjini kwa kukwama kwa maombi ya passport kwa miezi kadhaa iliyopita, maafisa wakidai ni tatizo la kimfumo na hawasemi lini litakuwa sawa hivo linaleta ukakasi kwa wananchi ambao wamefanya maombi ya passport waomba serikali iingilie kati suala hili.
 
Back
Top Bottom