LGE2024 Wananchi wahimizwa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 Tarime mji

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
23,905
27,826
26 September 2024
WANANCHI WAHIMIZWA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 TARIME MJI
thumb_991_800x420_0_0_auto.jpg
Posted on: September 26th, 2024
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Mji Tarime Bi Gimbana E Ntavyo amewaomba viongozi mbalimbali na asasi za kiraia kuwahimiza wananchi kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwakugombea nafasi mbalimba, kujitokeza kujiandikisha na kuwapigia kura viongozi bora

Hayo ameyasema leo kwenye ukumbi wa wa Halmashauri ya Mji wakati akitoa maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 katika Halmashauri ya Mji huku akisisitiza elimu ya mpiga kura ikitolewa kwa ufasaha wananchi watajitokeza wengi

"Sisi kwa umoja wetu kwenye maeneo yetu tukitoa elimu hii vizuri kwa wananchi naamini kabisa watajitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwani ni haki yao kikatiba kuanzia kugombea nafasi, kujiandikisha kwenye daftari kwa mtaa husika na kupiga kura siku ya tarehe 27, Novemba mwaka huu" amesema Gimbana

Aidha, amewataka viongozi hao pia wawashauri wanawake wenye sifa za kugombea katika jamiii kuja kuchukua fomu ili kuwania nafasi mbalimbali za Serikali za mitaa katika Halmashauri hiyo

"Zoezi la ugawaji fomu ni kuanzia tarehe 1 Novemba 2024 hadi tarehe 7 Novemba 2024 kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi kamili jioni Hivyo washaurini wanawake wenye sifa za kugombea kwenda kuchukua fomu pia za kugombea" amesema Gimbana

Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika tarehe 27, Novemba 2024, huku zoezi la wananchi kujiandika katika daftari la wapiga kura litaanza tarehe 11 hadi tarehe 20, Octoba 2024 katika mitaa yote 81 kutakuwa na vituo kuanzia majira ya saa 2 kamili asubuhi na kufungwa saa 12 kamili jioni kauli mbiu ni " Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, jitokeze kushiriki Uchaguzi
 
Tarime Mji
Tanzania

WADAU WANENA MAZITO BAADA YA KAULI YA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI DED Bi. GIMBANA E. NTAVYO KUZUMGUMZA


View: https://m.youtube.com/watch?v=N1rJy5Fahr4
Wadau hao kutoka taasisi za kijamii Tarime wataka mchakato ulio huru, wenye uwazi na utakaowezesha viongozi wanaotakiwa na wananchi kuweza kugombea na kuchaguliwa bila vizungiti vyovyote
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=EGDuDtcIZDo
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC , Bw. Kailima Ramadhani ameshiriki katika utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati huu wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ambapo pamoja na mambo mengine akiwa Kituo cha Bunda FM 92.1 kilichopo Wilaya ya Bunda Mkoani Mara, alieleza kwa kina Mambo matano yanayohusika katika uboreshaji wa sasa wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Mkoani Mara unataraji kuanza Septemba 04 hadi 10, 2024.
 
Back
Top Bottom