Wananchi waendelea kupatiwa msaada wa Kisheria kupitia Kampeni ya Mama Samia Legal Kampeni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,704
13,457
WhatsApp Image 2024-08-04 at 15.59.24_d4ddf930 (1).jpg
View attachment 3061527
Wananchi waendelea kupatiwa msaada mbalimbali wa kisheria kupitia Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Kampen iliyopo chini ya Wizara ya Sheria, katika kampeni hiyo watalamu wamepiga kambi kakitika Maonesho ya Nanenene, Jijini Dodoma.

Uwezo Maulid, Mkazi wa Shinyanga Mjini amesema “Mume wangu alikuwa Mtumishi wa Umma katika Manispaa ya Shinyanga, nilienda Mahakamani ili wanangu na mimi mwenyewe tupate haki kuhusu mali ya marehemu lakini sitendewi haki.

“Huu ni mwaka wa nne tangu marehemu afariki lakini mpaka dakika hii sijapata hata shilingi mia alizoacha, nyumba tuliyokuwa tunaishi nimefukuzwa na baba wa marehemu, nimekuja hapa ili nisaidiwe, mimi na wanangu tupate msaada wa kisheria na ninaamini nitasaidiwa.”

Luciana Mwanitu, kutoka Manispaa ya Dodoma, Kata ya Nzunguni amesema “Nimeelimishwa kuhusu huu mpango wa Mama Samia lakini nashauri jambo moja, hii ni Taasisi ni mpya na watu wengi hawaifahamu, hivyo ni muhimu sana kuongeza elimu hii katika maeneo mbalimbali ya Nchi hasa maeneo ya Vijijini.”

Pia, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa huduma ya elimu kupitia kampeni hiyo akisema ni huduma muhimu sana kwa Wananchi kwasababu wapo watu wengi wanashindwa kupata haki zao kwa kukosa msaada wa kisheria.

Upande wa Renatha Manda, amesema "Nashukuru sana nilikuwa na tatizo la Kisheria lakini nimekuja hapa nimepatiwa msaada wa Kisheria na tatizo limeisha.

“Pia nimepatiea ushauri na elimu nzuri kuhusu masuala ya kisheria na najipanga vizuri kwenye kuweka mirathi.”
 
Back
Top Bottom