Awali tuliambiwa kupitia tangazo la DAWASA kuwa maji yanatarajiwa kukatika Jumanne ya Julai 16, 2024 lakini jamaa wakakata huduma siku moja kabla.
Tangu wakati huo (Julai 15, 2024) mpaka muda huu naandika andiko hilo hakuna maji wala dalili ya maji.
Tumepiga simu sana na kwenda hadi ofisini kwao wanatuambia maji yatarejea kwa kuwa kuna bomba lilipasuliwa na watu wa TARURA waliokuwa wanakwangua Barabara.
Ni kweli hilo lilionekana, kwanza walichelewa kufika kwenye huduma ya kurekebisha bomba licha ya kutoa taarifa mapema, pili wamesharekebish tangu jana jioni lakini maji hakuna.
Ukiwapigia simu wanasema tu maji yatarudi, muda wowote bila kufafanua, hivi wao huko kwenye makazi yao wanaweza kuishi bila maji kwa muda wa wiki nzima?
Kibaya zaidi wale wanaouza maji kupitia magari wanakwambia hawauzi kwa tenki moja, lazima uanze na mawili ambapo kila moja ni SHILINGI 15,000.
Inamaanisha unatakiwa ulipie buku 30 kupata maji, haijalishi kama una tenki moja au hauna kabisa.
Hiki wanachokifanya sio sawa na hii sio mara yao ya kwanza hawa DAWASA KIBAHA kuwa na uzembe katika kuwajibika kuwahudumia watu inapotokea kuna bomba limepasuka au kuna changmoto nyingine yoyote inayohusisha maji kutoparikana
Majibu ya DAWASA ~
DAWASA yafafanua sababu za Wakazi wa Muheza Kibaha kukosa huduma ya maji kwa wiki nzima