Wananchi wa Arumeru waishukuru Serikali kwa kusambaziwa majiko ya gesi kwa punguzo la asilimia 50

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
876
2,373
Wakuu,

Inaonekana mambo ya nishati safi yameendelea kushika kasi hapa nchini

Wananchi wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha wameipongeza Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa mradi wa usambazaji na uuzwaji wa majiko ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50%

Wametoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti katika Kata ya Maji ya Chai Wilayani Arumeru Desemba 4,2024 wakati wa zoezi la uuzaji wa majiko hayo wilayani hapo.

WhatsApp Image 2024-12-08 at 16.06.03_311ee330.jpg

"Tunaipongeza Serikali kwa kuja na mpango huu; ambao unakwenda kutupunguzia madhara yanayosababishwa na matumizi ya kuni kupikia," amesema Joan Palangyo mkazi wa Kata ya Maji ya Chai.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza mradi wa kusambaza majiko ya gesi (LPG) ya kilo sita kote nchini ikiwa ni hatua ya kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao umelenga ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wawe wameachana na matumizi ya nishati isiyo safi na salama.

Source: Manara TV

=================

Wananchi Wilayani Karatu Mkoani Arusha wamejitokeza kwa wingi kujipatia majiko ya gesi ya kilo sita (LPG) yanayotolewa na Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya Lake Gas kwa bei ya ruzuku ya 50%.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wameipongeza Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuja na mkakati huo ambao wamesema utawasaidia kupunguza gharama walizokuwa wakitumia kununua mkaa.

Mkazi wa Kata ya Qurus, Neema Alfred amesema mkakati huo wa Serikali wa kusambaza majiko kwa bei ya ruzuku unakwenda kuwapunguzia adha ya kutembea mwendo mrefu kusaka kuni.

"Kijijini kwetu kuni hazipatikani ni hadi tutembee umbali mrefu; kwahiyo kupata haya majiko ya gesi na kwa bei nafuu ni neema kwetu," amesema Neema.

Elizabeth Fikalala kutoka Kiiiji cha Bashay alisema kijijini hapo upatikanaji wa kuni ama mkaa ni mgumu na kwamba wanalazimika kutumia gharama kubwa kunua mkaa hivyo ujio wa mradi huo ni mkombozi kwetu.

Naye Hassan Juma mkazi wa Kata ya Karatu ambaye anajishughulisha na uuzaji wa chipsi ameishukuru Serikali kwa kuwafikishia majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku na kwamba jiko hilo linakwenda kumrahisishia kazi zake.
WhatsApp Image 2024-12-08 at 16.06.05_8b24bedb.jpg

WhatsApp Image 2024-12-08 at 16.06.04_0fd530c1.jpg
"Tunaishukuru Serikali kwa hili la mitungi ya gesi, mazingira yetu yanakwenda kuwa masafi na pia ni rahisi kutumia tofauti na kutumia mkaa," alisema Juma.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao ulizunduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Mei mwaka huu.
 
IMG_20241208_174112_122.jpg

Serikali yawapa Wananchi majiko ya Gesi kwa bei ya ruzuku Karatu - Arusha, ni wale waliokuwa wakiteseka kwa upishi wa kuni

Wananchi Wilayani Karatu Mkoani Arusha wamejitokeza kwa wingi kujipatia majiko ya gesi ya kilo sita (LPG) yanayotolewa na Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya Lake Gas kwa bei ya ruzuku ya 50%.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wameipongeza Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuja na mkakati huo ambao wamesema utawasaidia kupunguza gharama walizokuwa wakitumia kununua mkaa.

Mkazi wa Kata ya Qurus, Neema Alfred amesema mkakati huo wa Serikali wa kusambaza majiko kwa bei ya ruzuku unakwenda kuwapunguzia adha ya kutembea mwendo mrefu kusaka kuni.

"Kijijini kwetu kuni hazipatikani ni hadi tutembee umbali mrefu; kwahiyo kupata haya majiko ya gesi na kwa bei nafuu ni neema kwetu," amesema Neema.

Elizabeth Fikalala kutoka Kiiiji cha Bashay alisema kijijini hapo upatikanaji wa kuni ama mkaa ni mgumu na kwamba wanalazimika kutumia gharama kubwa kunua mkaa hivyo ujio wa mradi huo ni mkombozi kwetu.

Naye Hassan Juma mkazi wa Kata ya Karatu ambaye anajishughulisha na uuzaji wa chipsi ameishukuru Serikali kwa kuwafikishia majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku na kwamba jiko hilo linakwenda kumrahisishia kazi zake.

"Tunaishukuru Serikali kwa hili la mitungi ya gesi, mazingira yetu yanakwenda kuwa masafi na pia ni rahisi kutumia tofauti na kutumia mkaa," alisema Juma.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao ulizunduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Mei, 2024.

IMG_20241208_174112_542.jpg

IMG_20241208_174112_122.jpg
 
Attachments

  • IMG_20241208_174112_556.jpg
    IMG_20241208_174112_556.jpg
    221.4 KB · Views: 3
Back
Top Bottom