View attachment 475178
Wapiganaji wa Kiislamu nchini Ufilipino wamechapisha kanda ya video inayoonyesha mateka mmoja wa Ujerumani akikatwa kichwa.
Jurgen Kanther alitekwa nyara katika jahazi lake pwani ya Malaysia jimbo la Sabah mnamo mwez Novemba.
Mwili wa mtu aliyekuwa naye baadaye ulipatikana katika mashua hiyo.
Siku ya mwisho ya kulipa fidia ya dola 483,000 ilikamilika siku ya Jumapili.
Bw Kantner mwenye umri wa miaka 70 na bi Merz walikuwa wamewahi kutekwa nyara awali.
Walizuiliwa kwa siku 52 mwaka 2008 na maharamia wa Kisomali na waliachiliwa huru baada ya kikombozi kutolewa.
Video hiyo ilioripotiwa na wapiganaji wa SITE inamuonyesha bwana Kantner akikatwa shingo na mtu aliyeshika kisu.
Mjumbe wa serikali Jesus Dureza alithibitisha mauaji hayo.
Hadi wakati wa mwisho sekta tofauti ikiwemo jeshi zilishindwa kuokoa maisha yake.
''Sote tulijaribu uwezo wetu lakini hatukufanikiwa'',alisema.
Abu Sayyaf ni kundi dogo na lenye ghasia kubwa kusini mwa Ufilipino, likijulikana kwa unyama wake ikiwemo kukata watu vichwa.
Kundi hio linatii wapiganaji wa Islamic State na limefanya utekaji nyara mwingi wa wageni na raia wa Ufilipino.
Wengine wamewachiliwa kwa kutoa kikombozi lakini idadi kubwa bado inaendelea kuzuiliwa.
Chanzo: BBC