Wanahabari tusitumike, nchi kwanza

Tulime

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
248
104
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) hawataki utaratibu,wamekataa kwenda na wakati,wamezoea kula bila kunawa.

TEF wametoa taarifa yao jana iliyoandikwa na kutajwa katika vyombo mbalimbali vya habari nchini hapa. Kwa maelezo ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti Theophil Makunga pamoja na Katibu wa Bodi hiyo Neville Meena imesema kuwa wametafakari kwa kina na kuazimia kutokubaliana na uamuzi wa uongozi wa Bunge wa kutokuonesha live vikao vya Bunge vinavyoendelea huko Dodoma.

TEF wamesema sababu za kufikia uamuzi ni tatu,
1. Kwamba habari zinachujwa mno kupitia utaratibu huu mpya wa FEED MAALUM.
2. Kwamba ubora wa picha unaorushwa na feed maalum ni duni mno.
3. Kwamba hatua hii inakwaza haki ya wanahabari ya kufanya kazi yao kwa uhuru zaidi.

Baada ya kupata taarifa hii ambayo inaweza kutafsirika kuwa ya msingi katika uhuru wa habari,nililazimika kuipitia tena taarifa ya Bunge juu ya utaratibu huu mpya wa urushaji wa Matangazo yake iliyotolewa na kitengo cha habari April 15,2016.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Bunge limeamua KUBORESHA mfumo wa urushaji matangazo yake kuufanya kuwa wa kisasa. Utaratibu huu umeelezwa kuwa ni utaratibu unaotumika na nchi nyingi wanachama wa jumuiya za Madola na kuwa utaratibu huu mpya utasaidia kupunguza USUMBUFU kwa Bunge na Wanahabari kwa kupunguza mzigo wa kutembea na vifaa,badala yake taarifa itawafikia moja kwa moja katika maeneo yao kupitia masafa marefu(frequencies)itakayorushwa na sattelite ya Intelsat ya 17 iliyo nyuzi 66 mashariki kwa masafa maalumu.

Kwa bahati mbaya TEF wameukataa utaratibu huu bora na wa kisasa. Hawataki kwenda na wakati kwa sababu dhaifu ya haki ya kupashana habari. Wahariri wa Tanzania wanatamani haki zaidi ya wajibu,TEF wanataka kutuaminisha kuwa haki hii kwa Tanzania ni muhimu kuliko nchi zote wanachama wa jumuiya ya madola. Wahariri wetu wameacha kutumia taaluma zao badala yake wanafanya kazi kwa maelekezo ya Freeman Mbowe.
Yuko wapi Mhariri makini asaidie kufanya utafiti katika nchi nyingine zinazotumia utaratibu huu,aainishe kasoro zake ambazo kwetu ni kubwa kuliko kokote Duniani?

TEF wamesema wanaukataa utaratibu huu kwa kuwa habari zinachujwa mno! Hawa ndio wahariri wasiojua majukumu yao. Akili za kupewa changanya na za kwako,TEF wamesahau kuwa jukumu lao kubwa ni kuchuja habari ili kwendana na utamaduni na miiko ya Nchi yetu. TEF wanashangaa Bunge kuchuja habari kwa mujibu wa taratibu na hadhi ya Bunge.

TEF kwa kujua ama kutojua wameshirikishwa kuandaa mgogoro mkubwa zaidi katika Nchi yetu. Tunapaswa kuepuka Siasa za mazoea ili Taifa lisonge mbele kwa kuwa sasa ni sharti tufanye siasa kwa vitendo kusaidia kuharakisha maendeleo katika nchi yetu na hii ndio sababu nawashauli ndg zangu wahariri wajitenge na siasa za kihuni za Freeman Mbowe.

Mwaka 2007, Freeman Mbowe aliwatumia waalimu kisiasa,wakagoma nchi ikapatwa na janga katika sekta ya elimu,hasara ambayo bado kwisha hadi sasa kwani ni baada ya hapo ndipo tukaanza kusikia katika nchi hii mwanafunzi anamaliza darasa la saba hajui kusoma.

Mwaka 2012, Mbowe aliwatumia vibaya madaktari akiwamo Katibu mkuu wa sasa wa Chadema,nchi ikapatwa na maafa haikupata kutokea tangu tupate uhuru. Watu wakafa kwa kukosa huduma kisa madaktari wamegoma,tuliopoteza ndugu zetu,tukaumia,tukalia,ikatoka hivyo na kuiacha mioyo yetu imevimba kwa kisasi hadi sasa.

Mwaka huu Mbowe ameanza chokochoko na tasnia ya habari. Anadhamiria kuwatumia vibaya wahariri na waandishi ili kuharibu mtiririko wa mafanikio makubwa yanayoendelea kuonekana katika awamu hii ya tano chini ya Rais John P. Magufuli. Mbowe anakusudia kuwafitinisha waandishi wa habari na Serikali yao,ikumbukwe kuwa Vyombo vya habari ni muhimu kwa ustawi wa Taifa lolote Duniani. Ikiwa waandishi wa habari watatumika vibaya nchi hutawalika kwa taabu sana.

Ndugu zangu Wahariri,utaratibu wa hapa kwetu ni kunawa kabla ya kula. Imezoeleka hivo!
Tunawe kisha tule,tuache siasa tufanye taaluma ili nchi yetu isonge mbele.
#NCHI YANGU KWANZA.
 
Kwa kuzuia matangazo ya bunge ccm imefanya kosa la kiufundi kama ilivyofanya kwenye katiba mpya, kwa sasa mnaweza msilione na mkajisifia kwamba mmewashika lkn ina a long run hili halitakuwa na impact nzuri kwa chama. Time will tell.
 
Hatutaki uhuni unaofanywa na serikali ya viwanda,haiwezekani bunge kuendeshewa chumbani,tunataka kuliona bunge live.Kwa nini wao kila wanachokifanya wanataka kuonekana kweny makamera lakini hawataki na sisi tuone kile tunachokitaka.Hili suala halikubaliki!!
 
Wewe ni msemaji wa serikali na bunge? Maana hapa unawasemea kama vile wamekutuma. Na majibu yenyewe sio majibu bali mashambulizi kwa Mbowe, wewe ni nani kumshambulia Mbowe kwa uzushi wako?
Kwa kawaida watu wenye akili timamu wanapoona mtu kasimama hadharani bila woga wala kujificha na anakosoa dola huwa wanakaa pembeni na kutafakari sana hoja hizo badala ya kubishana bila akili kama hivi ufanyavyo.
Ogopa sana wasio na tabia za kujipendekeza, hao ndio WATU kwa maana ya WATU.
Iacheni serikali inao wasemaji wake, msiongeze pumba juu ya pumba. Mtaweka wapi sura zenu kesho serikali ikikubaliana na kuwa Bunge ni " NATIONAL ASSEMBLY"? na haitakiwi usiri?
 
Kwa kuzuia matangazo ya bunge ccm imefanya kosa la kiufundi kama ilivyofanya kwenye katiba mpya, kwa sasa mnaweza msilione na mkajisifia kwamba mmewashika lkn ina a long run hili halitakuwa na impact nzuri kwa chama. Time will tell.
Binafsi katika hili la kuzuia bunge live,hata kama serikali hii itafanya jema gani,ntaichukia milele daima
 
Kwani Tanzania inawajibika kuiga mambo ya nchi nyingine?

Upo wapi huo usasa wa teknolojia ilhali picha ni duni?

Kwa wema gani eti kumpunguzia mwandishi mzigo wa kubeba kamera, tangu lini mkia ukawa mzigo kwa kondoo?

Mwanzo hoja ilikuwa gharama, leo yamekuwa ya teknolojia. Hivi nikienda kunyolewa na kiwembe chini ya mti si chaguo langu?

Sasa wamekuwa ya Mbowe, mbona wewe unataka tufuate ya madola?
 
Uliyeandika waraka huu, una tatizo kubwa na unahitaji msaada. Hebu nikuulize, Bunge linahofu nini waandishi wa habari kurusha matangazo watakavyo?

Huo utaratibu unaopewa jina Jumuiya ya Madola ni kiini macho tu. Hivi mwenzako akinya sebuleni na wewe utakunya ili ufanane naye? Utaratibu wa jumuiya ya Madola ni movie na ndio ukoloni tunaoukataa.
Halafu hapa usimwingize Mbowe, kwa sababu huna ushahidi kwamba anawatumia waandishi was habari, kama unao ulete. Tunachodai ni haki ya wananchi kupata habari kwa mujibu was ibara ya 18 ya katiba.
 
Huyu ni mpambe tu, Hata Maguguli hamjui
 
Wanafiq hawakosekani
 
LAKINI tuache ushabiki wa vyama hali ya BUNGE letu lililopita ilikuwa aibu kwa Waheshimiwa wabunge wetu maneno ambayo walikuwa wanatupiana heshima ilipotea sasa yale kwa kweli kuonekana hadharani AIBU AIBU tuache tu ihaririwe yale maneno ya mipasho ya kina AISHA MASHAUZI na MZEE YUSUPH wayasikie wenyewe tu humo ndani sisi hatuyahitaji kutuharibia jamii.
 
Kafie mbali na pumba zako. Wee unafikiri wanachofanya kuzuia uhuru kwenye hii era ya information ni sahihi. Mnaturudisha zama za mawe?

Kwamba wanaotakiwa kupata habari ni viongozi tu basi?

Hebu acheni hizo bana... Hv serikali ya magu inaogopa nini? Inabidi tuanze kujiuliza kwa kweli...
 
Unajua ukitaka kujua vema linganisha na mabunge mengine duniani. Tumia muda wako uwe unatazama ndio utajua bunge la Tanzania kumbe ni la kistarabu sana.
Pale South Afrika Rais anahutubia bunge na wanamkatiza na kumwita mwizi, fisadi na mengine. Jee kwetu laweza kutokea hilo? Ukraine, Kenya na kwingine ngumi zinapigwa watu kutetea misimamo yao sasa sisi vijembe tuu vinakusumbua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…