Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,782
- 13,541
Zaidi ya wanafunzi 21,930 wa Shule za Msingi Mkoani Mwanza bado hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu hivyo walimu kutakiwa kuongeza jitihada na mbinu zitakazofanikisha wanafunzi kumaliza darasa la kwanza wakiwa na stadi hizo za KKK tatu.
Akizungumza na Walimu na wasimamizi wa masuala ya elimu mkoani hapo wakati wa kikao kazi cha mapitio ya tathmini ya utekelezaji wa shughuli ya uboreshaji na usimamizi wa elimu, Waziri wa TAMISEMI, Angellah Kairuki amesema idadi hiyo ni kubwa na inapaswa hatua za haraka kuchukuliwa.
Amesema: “Kuendelea kubaki na kiwango hichi cha zaidi ya Watoto 21,930 wa shule za msingi wasiokuwa na stadi hizo tatu hatua za haraka zichukuliwe.
“Kila mmoja kwa nafasi yake anatakiwa kufuatilia namna gani Walimu wetu wanapokuwa darasani viwango vyao vya ubora na viwago vya ufundishaji, pia tuendeee kutatua kero za Walimu wetu katika vituo vya kazi.