Hilo tatizo kwa dsm ni kubwa,bahati mbaya wanafunzi wa msingi hubeba madtari yote kila siku,umbali ukiongeza lundo la madfari mateso matupu,hapa wazazi wenyewe chanzo cha yote,wazazi wengi wapo bize na majukumu mengine hawana muda wa kubaini,nakushukuru kwa mtoa uzi angalau umeliona hili.Hili suala linawahusu sana wanafunzi wa shule za msingi, na kama tujuavyo siku hizi mwanafunzi wa kiwango hiki cha elimu anakua na umri mdogo sana hasa akiwa madarasa ya chini...
Unatoka kazini jioni na kukutana na watoto wengi wakiwa wanagombania usafiri, kitu ambacho ni hatari kutokana na umri wao. Kama hilo la kugombania usafiri halitoshi pia wanakutana na kadhia ya foleni...
Mtoto anaishi gongolamboto lkn anasoma sinza. Mtoto huyu anachelewa kurudi nyumbani na akirudi anakua amechoka sana, anajisomea saa ngapi?
Hivi haiwezekani kuweka utaratibu wa kusoma maeneo wanaoishi hasa kwa hawa wa shule za msingi?
Tuwaangalie watoto hawa.
Nadhani tatizo linatokana na maeneo yenye wakazi wengi kutokuwa na shule nyingi.Sasa hivi ukienda pembezoni mwa mji makazi ya watu yanakuwa Kwa Kasi lakini huoni maeneo ya shule yakitengwa.Baada ya muda unakuja kuta Eneo limeshakuwa na wakazi wengi lkn shule hazipoHilo tatizo kwa dsm ni kubwa,bahati mbaya wanafunzi wa msingi hubeba madtari yote kila siku,umbali ukiongeza lundo la madfari mateso matupu,hapa wazazi wenyewe chanzo cha yote,wazazi wengi wapo bize na majukumu mengine hawana muda wa kubaini,nakushukuru kwa mtoa uzi angalau umeliona hili.
Sijui wazazi wanajisikiaje,upo zako kwenye mishe zako halafu unamuacha mtoto mdogo aende umbali mrefu hivyo tena apambane kwenye daladala.Hilo suala huwa linanisononesha sana.
Yaani unaweza ukaona katoto kadogo kweli halafu kako peke yake tu kanasubiri kupanda daladala.
Hii jamii yetu ina dosari nyingi mno kwa kweli.
Mimi siwezi kabisa kumwacha mtoto wangu ahangaike na madaladala peke yake.
Hii ni shida kubwa,ndiyo maana matokeo ya mitihani Huwa sio mazuri sanaTatizo ni nyumba zenu za kupanga.
Mnahamahama sana January upo Tegeta, Mwezi march umehamia Mbagara August upo Sinza.
Kwa jinsi mnavyohamahama mnawatesa watoto wenu
Yap kitu cha kwanza ni Usalama.Lakini hata umbali ni tatizo kubwa.Kuna mtoto alikuwa anaishi na wazazi wake Kivule na alikuwa anasoma Kivule (Kitunda Kwa mbele).Wazazi wake wakatengana ikabidi mtoto akaishi Kwa Mzazi mmoja Mbezi Tangi Bovu.Just Imagine hii route ya Kivule to Tangi bovu tena Kwa daladala ni mateso makubwa.MUHIMU Ni kuangalia usalama wao ilo la umbali siyo tija.
Jambo lingine, hata hizo shule wakisema waandikishe watoto wa jirani na shule hiyo hawawezi kutosheleza hata madarasa mawili.