Wanafunzi waliopata mimba wakiwa shuleni wana haki ya kuendelea kusoma

LENGISHO

Senior Member
Sep 15, 2017
169
245
Leo asubuhi nikiwa najiandaa kuelekea katika shughuli zangu za kila siku nikiwa nimefungua Radio free kusikiliza yaliyojiri magazetini ,kabla ya kipindi kuanza palipita tangazo , tangazo hilo ni mwanafunzi alikuwa Analia kwa sababu amepatiwa mimba na hawezi kwenda tena shulen kwasababu ya ujauzito, katika tangazo hilo bibi yake amesikika akimfariji na umwambia “ Usilie maana kijiji kizima kinafahamu kuwa wewe ulibakwa ndio ukapata mimba kutokana na umbali wa shule uliyokuwa unaenda” Mwisho wa kunukuu
Nilikaa nikatafakari sana je katazo la kusomesha wanafunzi wote waliopata mimba n sahihi?

Nikatafaari mbali sana zaidi , Mzazi anapompeleka shuleni mwanae huwa anategemea mtoto huyo atakuja kumsaidia kwa maisha ya baadae kwa hiyo mzazi hutumia rasilimali nyingi kuhakikisha mwanae anasoma na kutimiza ndoto zake kwa maisha ya baadae.

Mtoto huyo aliyeachishwa masomo kwa kupata mimba na kukosa haki yake ya kimsingi ya kuenelea kusoma kama ilivyoainishwa katika katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza Haki ya kufanya kazi, kupata elimu na nyinginezo Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 “ Kila mtu anayo haki ya kujielimisha, na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.”

Pia inaendelea kutia msisitizo katika kifungu kidogo cha 3 kuwa “ Serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo vinginevyo vya mafunzo” Hivyo basi kutokana na Mtoto huyo kunyimwa haki yake ya kimsingi anapelekea kwa maisha ya baadae kuzalisha jamii maskini ki kipato ,na kifkira.

Mfano mzuri wazazi wa mtoto huyu watakata tamaa kusomesha watoto wa kike wakihofia kupata mimba hivyo basi kama mtoto huyu alikuwa ajekuwa mtu wa aina flani hivyi ambae angeikomba jamii ndoto zake zimefia hapo hapo kwa kutojitakia hivyo dhana ya ubaguzi wa jinsia kurudia enzi zake.

Pili Mtoto huyu aliyeacha shule kwa mimba atazaa mtoto na atashindwa kumlea ipasavyo kutokana na kukosa elimu , madara yake watoto wa mitaani wataonezeka ,vibaka wataongezeka , wezi na wakabaji wataongezeka .
Nimeenda zaid na kuwaza tena ivi ni kweli waliopata mimba wote wakiwa mashuleni chanzo ni hao kujitakia ? je sababu za mimba kwa wanafunzi ni tamaa zao tu ? mbona mkuu aliacha kuconside factor kama vile jografia ya eneo ambalo mwanafunzi amepatia mimba Mfano unaweza kuta mtoto anatembea Km 3 had 5 kwenda shulen hapo njian akielekea na wakati wa kurudi shulen n mjaribu mangapi anayapitia ? je kama serikali ingejenga shule karibu na makazi yake angepata mimba ?

NB:
HAKI HAIOMBWI INADAIWA
FB_IMG_1626157031636.jpg
 
Ajifungue kwanza ndo aendelee na masomo ikiwezekana. kibinti kama paula kajala kumtetea aendelee na masomo baada ya kukitembeza kwa sana ni kupoteza muda na rasimali mbalimbali
 
Back
Top Bottom