Wanafunzi waliofariki Lucky Vincent watunikiwe vyeti vya kumaliza elimu yao (Posthumous certificate)

wehoodie

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
1,030
1,010
Simanzi na majonzi vimeukumba mji wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kufuatia ajali iliyosababisha vifo vya wanafunzi wa darasa la 7 wa shule ya Lucky Vincent. Wanafunzi hawa walikuwa wanakwenda kufanya mtihani wa Moko (mock) ili kujiandaa na mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi.

Napendekeza mamlaka husika kuwatunikia vyeti vya heshima vya kumaliza elimu ya msingi kutambua utayari wao wa kumaliza elimu hiyo na kuenzi pia juhudi zao za kupata elimu. Cheti/vyeti hivyo wanaweza pewa wazazi au shule yao kama kumbukumbu.

Vyeti hivi vya 'Posthumous' hutolewa nchi za wenzetu. Mfano Hivi karibuni chuo kikuu cha Florida kitampatia kijana Tryvone Martin alieuwawa mwaka 2012 shahada ya sayansi ya anga (Bachelor degree in aviation science) ambapo wazazi wake watapokea kwa niaba yake.

Poleni sana wazazi, wanafunzi, waalimu na jamii nzima ya wafiwa kwa msiba huu.
 
Wameitwa tuwaache,ila kama kuna picha zao tuzione ili tuwaombee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…