Wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi wakamatwa na bunduki.

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Nairobi bewa la lower kabete wamekamatwa kutoka katika chumba chao cha kulala wakihusishwa na uhalifu wa kutumia silaha katika eneo hilo.

Inasemekana kwamba wanafunzi hao wamekuwa wakivamia nyumba za watu na kuwaibia.

Wakaazi wa kabete wakishirikiana na polisi waliamua kufanya msako katika vyumba vyao vya kukodisha ambapo bunduki moja ya kujitengenezea na misokoto kadhaa ya bangi imepatikana kutoka katika vyumba vyao.

Taswira waliokumbana nayo polisi hapo,niliashiria kuwa wanafunzi hao hawakuwa wa kawaida jinsi alivyoafki mkuu wa polisi wa kituo cha Kikuyu Brigian Kiptoo.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…