KERO Wanafunzi Teofilo Kisanji University (TEKU) hatujapata vyeti vyetu vya digrii 2024 hadi leo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Jan 14, 2025
31
62
Habari za muda huu

Sisi kama wanafunzi wa digrii tuliomaliza chuo mwaka Jana 2024 katika chuo kikuu TEOFILO KISANJI tunamalalamiko juu ya kile uongozi wa chuo unavotufanyia watahiniwa wake kuhusu vyeti vyetu ambapo Hadi Leo tarehe 29/1/2025 hawajatupa vyeti vyeti na hawajatoa au kutupa taarifa yeyote rasmi kua vyeti vyetu tunapata lini?

Jambo Jingine ni kwamba katika ulimwengu huu wa ajira cheti hasa cha chuo kikuu ni muhimu na sifa mojawapo kwa kijana kupata kazi kutokana na ushindani uliopo katika ajira hivo tunaomba uongozi wa chuo utupe majibu ya kueleweka kwamba vyeti vyetu tutapata lini.
 
Back
Top Bottom