Wanafunzi SUA walia na bodi ya mikopo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,717
55,819

Wanafunzi 204 wakozi tofauti katika chuo kikuu cha sokoine cha kilimo SUA wako hatarini kushindwa kuendelea na masomo kufuatia bodi ya mikopo kushindwa kuliwapa feha za mikopo kwa madai kuwa hawajapeleka vielelezo vyao licha ya serikali ya wanafunzi kuwasilisha vielelezo hivyo hali inayosababisha wanafunzi hao kuishi kwa tabu chuoni.

Akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho Osca Ndunguru ametupia lawama bodi ya mikopo kuendelea kuwatesa wanafunzi huku wanafunzi hivyo amemuomba rais Magufuli kutembelea bodi ya mikopo kuchunguza uozo unaofanyika na kwamba bodi hiyo ihakikishe inashugulikia tatizo la wanafunzi hao ndani ya siku tatu.

Nao baadhi ya wanafunzi walioathiriwa na tatizo la kukosa mikopo wameeleza kusikitishwa kwao na kwamba wanalazimika kuishi kwa tabu kwa kukopeshana wanafunzi kwa wanafunzi wakitegemea bodi ya mikopo itawalipa fedha zao lakini kadri siku zinavyozidi kusonga mbele hali ya maisha yao chuoni yanazidi kuwa magumu.

Waziri mkuu wa serikali hiyo ya wanafunzi amesisitiza na kuiomba serikali ya rais Magufuli kuangalia upya mfumo wa utendaji wa watumishi wa bodi ya mikopo kwani wanafanya kazi hiyo kwa mazoea na upendeleo kwa baadhi ya watu hali inayozorotesha maendeleo ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…