KERO Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Morogoro hatujalipwa fedha zetu za refund toka mwaka 2023 licha ya Uongozi wa Chuo kuahidi kushughulikia Septemba 2023

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Rejea kwenye mamaliko ya uzi huu - Chuo Kikuu cha Mzumbe chakiri Wanafunzi zaidi ya 500 wanadai malipo ya 'refund' chuoni hapo

Hadi Leo hii pesa zetu bado hatujalipwa na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa zaidi ya kuzungushwa tu.

Tunaomba mtusaidie wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Morogoro jamani, licha ya kuandika barua tangu mwezi wa tisa 2023 lakini hakuna malipo yoyote yaliyofanyika.

=====

Ufafanuzi kutoka Kitengo cha Mawasiliano Chuo cha Mzumbe (Juni 3, 2024)

JamiiForums imefanya mawasiliano na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Lulu Mussa amesema;

Madai ya nyuma yameshalipwa kama tulivyofafanua wakati huo, hadi waliohitimu chuo Novemba 2023 wameshalipwa, ambao hawajalipwa ni wenye madai mapya.

Jumla ya wanaodai ni 1,075, ili uweze kulipwa lazima uhakiki ufanyike, waliofanyiwa uhakiki hadi sasa ni 611, waliosalia ni464 bado uhakiki haujafanyika.

Hivyo, wanaodai na ambao uhakiki wao umeshafanyika watalipwa lakini siwezi kusema ni lini, hao ambao bado hawajafanyiwa uhakiki pia watalipwa mchakato ukikamilika.
 
Inawezekana labda kuna shida mahali au umejichanganya hamna unachodai. Nawafahamu watu wengi sana waliomaliza 2023 wameshalipwa hela zao.
 
Rejea kwenye mamaliko ya uzi huu - Chuo Kikuu cha Mzumbe chakiri Wanafunzi zaidi ya 500 wanadai malipo ya 'refund' chuoni hapo

Hadi Leo hii pesa zetu bado hatujalipwa na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa zaidi ya kuzungushwa tu.

Tunaomba mtusaidie wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Morogoro jamani, licha ya kuandika barua tangu mwezi wa tisa 2023 lakini hakuna malipo yoyote yaliyofanyika.

=====

Ufafanuzi kutoka Kitengo cha Mawasiliano Chuo cha Mzumbe (Juni 3, 2024)

JamiiForums imefanya mawasiliano na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Lulu Mussa amesema;

Madai ya nyuma yameshalipwa kama tulivyofafanua wakati huo, hadi waliohitimu chuo Novemba 2023 wameshalipwa, ambao hawajalipwa ni wenye madai mapya.

Jumla ya wanaodai ni 1,075, ili uweze kulipwa lazima uhakiki ufanyike, waliofanyiwa uhakiki hadi sasa ni 611, waliosalia ni464 bado uhakiki haujafanyika.

Hivyo, wanaodai na ambao uhakiki wao umeshafanyika watalipwa lakini siwezi kusema ni lini, hao ambao bado hawajafanyiwa uhakiki pia watalipwa mchakato ukikamilika.
Sisi tuliomaliza masomo yetu katika Chuo Kikuu cha St. John's pale Dodoma hadi leo hatujawahi kupewa ufumbuzi wowote kuhusu marejesho yetu. Hata tangazo rasmi halijawahi kutolewa, licha ya wadau kwenye jamii forums kuibua suala hili. Tumevunjika moyo kabisa.
 
Back
Top Bottom