Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 520
- 2,929
Mh. Rais Samia ,Waziri wa Elimu Prof.Mkenda na Wizara ya Elimu kwa ujumla kwanza napenda kupongeza mfumo huu Mpya wa Samia Scholarship ulioanzishwa kutoa ufadhili wa Masomo vyuo vikuu 100% kwa wanafunzi wa Masomo ya Sayansi waliofanya vizuri kidato cha 6 na wanaokwenda vyuo vikuu kusomea Sayansi,Uhandisi na Elimu tiba .
Ni Mfumo wa ufadhili mzuri ila wenye mapungufu. Mbali na pongezi hizo nilizotoa lakini naomba kuonesha mapungufu ya Mfumo huu wa ufadhili na mapendekezo yangu.
Wanafunzi waliobahatika kupata Samia Scholarship ni wale tuu waliofanya vizuri sana kwenye masomo ya Sayansi katika Matokeo ya kidato cha Sita. Na wizara inawachambua na kuweka wazi majina yao kwenye tovuti kwamba wamekidhi vigezo vya kuomba Samia Scholarship kwa sharti ya kwamba vyuo vikuu wakasome Sayansi , Uhandisi,Hisabati au Elimu Tiba.
Mwaka jana ,Mwaka wa Masomo 2022/2023 takribani wanafunzi 640 walipata ufadhili wa Samia Scholarship katika vyuo mbalimbali nchini . Baada ya wanafunzi hawa kupata ufadhili kuna mkataba wanasaini na serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Mkataba huu una masharti ya kwamba Mwanafunzi anayepata Samia Scholarship katika Matokeo yake ya Mwaka hapaswi kupata chini ya GPA ya 3.8 , chini ya GPA ya 3.8 mwanafunzi huyo anaondolewa katika ufadhili wa Samia Scholarship.
Kwa Matokeo ya Mwaka wa Masomo 2022/2023 ulioisha kati ya wanafunzi 640 waliopata Samia Scholarship ambao sasa wanaingia Mwaka wa pili wa masomo 2023/2024 ni wanafunzi 222 tuu ndio waliopata kuanzia GPA ya 3.8 ila wanafunzi 238 kati ya 640 wamepata chini ya GPA ya 3.8, ambapo moja kwa moja wameondolewa kwenye ufadhili wa Samia Scholarship.
Na hadi sasa wanafunzi hawa 238 hawajui hatma yao ,ambapo kati yao wanafunzi 173 wamepata GPA ya 3.5 hadi 3.7 na waliobaki wamepata GPA chini ya 3.5. Na vyuo vimefunguliwa na vyuo vingi usajili wa Masomo unaisha tar.10/11/2023 hawa wanafunzi wapo dilema ,hawajui hatma yao .
Waziri wa Elimu Mzee wangu ,Prof.Mkenda aliwahi sema wanafunzi waliopata chini ya GPA ya 3.8 wataingizwa kwenye mikopo ya kawaida ya Bodi ya Mikopo (Heslb) ,Bodi ya Mikopo hadi sasa wanasema hawana hiyo taarifa ya hao wanafunzi kupewa mikopo ya kawaida sababu dirisha limefungwa ,na wao wanafuata miongozo , taratibu na sheria zilizopo za utoaji mikopo.
Kuna jambo halipo sawa hapa ambalo nina shauri serikali kuchukua hatua za haraka ili kusaidia wanafunzi hawa,na ushauri wangu ni huu.
1. Mbali na dhamira ya serikali kuweka kiwango cha GPA ili mwanafunzi azidi kufaulu vizuri ila GPA ya 3.8 ni kubwa, ukizingatia mazingira ya vyuo vyetu nchini ni tofauti. Nina shauri serikali GPA iwe kuanzia Upper Second 3.5 . Sababu wanafunzi waliopata kuanzia GPA ya 3.5 hadi 3.7 ni 173 kati ya hao 238 .
2. Serikali iondoe Mfumo wa sharti ya kupata kiwango cha GPA fulani ili kuendelea kufadhiliwa chuo kikuu isipokuwa tuu kwa wanafunzi watakao Disco au kuacha masomo .Sifa za awali kufaulu vizuri kidato cha sita masomo ya Sayansi na kusomea Sayansi, Uhandisi, Hisabati au Elimu Tiba sifa hizi zinatosha.
3. Au serikali iweke sharti ya Kiwango cha GPA ya ujumla baada ya mwanafunzi kumaliza masomo yake miaka yote (Overall GPA ). Kama kiwango ni GPA ya 3.8 iwe GPA ya Jumla (Overall GPA) baada ya kumaliza masomo miaka yote chuoni na sio calculation ya GPA ya Mwaka. Mwanafunzi ambaye atafikisha Overall GPA fulani aidha 3.8 au 3.5 basi ni ufadhili kwake serikali ilimsomesha bure kupitia SAMIA SCHOLARSHIP na kama Mwanafunzi hatafikisha GPA iliyokusudiwa aidha 3.8 au 3.5 basi iwe amesomeshwa kwa mkopo na atapaswa kuulipa,ingawa binafsi napendezwa na njia ya kufuta sharti la kupata GPA fulani ili kufadhiliwa .
4. Serikali iliahidi wanafunzi waliopata chini GPA 3.8 na kuondolewa ufadhili wa Samia Scholarship watapewa mikopo ya kawaida kupitia Bodi ya Mikopo. Hadi sasa hakuna kilicho ratibiwa .
Bodi ya Mikopo wanasema hawana hiyo taarifa kwani wao wanafuata taratibu na miongozo, ambapo mwanafunzi anatakiwa kuomba ili kupata mkopo na hadi sasa dirisha la maombi limefungwa.Pili mwanafunzi awe na vigezo (awe hana uwezo ) ambapo kwenye Samia Scholarship hawangalii kigezo cha uwezo wa kugharamia bali ufaulu kidato cha Sita kwa wanafunzi wa Shule zote binafsi au serikali hivyo wao wanashindwa kujua wenye uwezo na wasio na uwezo kwenye Samia Scholarship sababu hawana taarifa zao,hivyo hawawezi kuwahamishia kupata mkopo wa kawaida moja kwa moja.
Nina shauri kama kuwahamishia mkopo wa kawaida kupitia HESLB haiwezekani kirahisi ,Serikali kwa sasa ichukue pendekezo namba 2 kufuta sharti la kupata kiwango fulani cha GPA ili kuendelea kufadhiliwa isipokuwa tuu kwa wanafunzi walio Disco au kuacha Masomo ndio ufadhili usitishwe.
Na kwa mtanzuko huu, naona umuhimu wa mawazo ya ACT WAZALENDO kwenye Ilani ya uchaguzi wa 2020 kurasa wa 21 na 22 ,kwamba ACT wazalendo tukipata ridhaa ya kuunda na kuongoza serikali tutalipa Ada (Tuition Fee) bure kwa wanafunzi wote wanaodahiliwa chuo kikuu ,fedha ya field bure ,fedha ya vitabu bure kwa wanafunzi wote.Mkopo utakuwa tuu kwa fedha za kujikimu tuu (Meals and accomodations) na hii wanafunzi wote watakaomba watapata .
Ahsante.
Abdul Nondo.
Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Taifa -ACT Wazalendo.
Taarifa zaidi kuhusu Wanafunzi hao soma hapa - Taarifa kwa Wanafunzi 238 wa Samia Scholarship 2022/2023 kupata mkopo wa Bodi ya Mikopo