Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,168
- 5,523
Aggness Daniel (Aggy Simba)
Dkt. Mohammed
Sekretarieti ya Klabu ya Simba imewafungia kujihusisha na masuala ya klabu Wanachama Mohamed Khamisi Mohamed maarufu Dr. Mohammed na Agnes M. Daniel maarufu Aggy Simba mpaka pale kamati ya maadili itakapoamua vinginevyo.
Sekretarieti imepokea malalamiko mengi ya kimaadili dhidi ya Wanafamilia hao wa klabu ya Simba ikiwemo kuitisha mikutano kinyume na taratibu na kuchochea migogoro ndani ya Klabu.
Sekretarieti itawafikisha Wanachama hao mbele ya Kamati ya maadili hivi karibuni.
Uamuzi huo umefikiwa kwa Mamlaka ya Sekretarieti iliyonayo chini ya Ibara ya 31(4)(g) ya katiba ya Simba ya klabu ya 2018 (kama ilivyofanyiwa mareke- bisho 2024), katika kuhakikisha Mahusiano ndani ya Klabu, Wanachama, na Mashabiki hayaathiriwi.
Sekretarieti inawakumbusha wanachama na mashabiki kuheshimu Katiba, Kanuni, na Miongozo iliyopo ndani ya Klabu.
Imetolewa na Sekretarieti, Simba Sports Club Juni 15, 2024
Simba SC kumekuwa na sintofahamu nyingi, soma mada hizi kuelewa kinachoendeea:
- Wajumbe Bodi ya Simba upande wa Wanachama wagoma kujiuzulu
- Salim Abdallah 'Try Again' ajiuzulu uenyekiti bodi ya wakurugenzi Simba
- Bodi ya Simba upande wa mashabiki wanataka kumtapeli Mo Simba yake
- Tetesi: - Simba imepasuka. Kuna Simba ya Try Again na Simba ya Mo, Kila upande unauroga upande mwingine
- Tetesi: - Simba inatarajia kumrejesha tena Barbara Gonzalez kwenye Bodi
- Hivi lile sakata la baadhi ya mashabiki wa simba kumshinikiza Mwenyekiti wao Mangungu kujiuzulu, limefikia hatua gani mpaka sasa?