WANACHAMA CHADEMA MBEYA WATIMKIA CCM
MBEYA: Zaidi ya Wanachama wapya 50 wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Mbeya kutoka katika vyama vya upinzani wakitaja kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kuwa sababu ya kukiamini na kuamua kujiunga na chama hicho.
Wanachama hao wapya wamejiunga na CCM leo Machi 27,2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Ruanda Nzovwe Wilaya ya Mbeya ya Mjini mkoani Mbeya ikiwa ni mwanzo wa ziara ya siku tatu
Katibu wa Halmashauri Kuu(NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla katika mikoa miwili ya Mbeya na Iringa.
Aidha, Makalla aliwapongeza wanachama hao kuhamia CCM kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kutoa kwa maelekezo kwa katibu wa Mkoa na Wilaya kuwaweka katika utaratibu na usajili mzuri wa CCM kwani wanakwenda kuongeza idadi ya wanachama waliopo katika chama hicho.
“Hawa ni wanachama wanakwenda kuongeza idadi CCM ndiyo chama kikubwa kinachoongoza kwa wanachama wengi na kushika namba moja Afrika na kushika namba saba kwa dunia nzima, CCM inawanachama milioni 12 na leo inasoma milioni 12,000,050 nguvu ya chama ni wafuasi wake na hawa tunaongeza jeshi na kukisaidia chama,” amesema Makalla.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Moja ya wanachama wapya waliojiunga na CCM, Jackson Simon amesema amehama chama hicho kutokana na mambo makubwa aliyoyaona yamefanywa na CCM na wapo tayari kuungana na chama kwa ajili ya maendeleo ya taifa kwa ujumla.