Siku hizi, baadhi ya wanaCCM wajinga wamekuwa wakiangamiza CCM, huku wenyewe wakiamini wanaisaidia.
Siku hizi, mara nyingi mtu akiongelea haki au demokrasia, wanaCCM hao wajinga utawasikia wakimsema mtu huyo ni CHADEMA.
Hata kiongozi wa dini akiongelea tu suala la haki au demokrasia au kupinga ufisadi, wanaCCM hao wajinga utawasikia wakimsema kuwa kiongozi huyo atakuwa ni CHADEMA.
Tafsiri yake, kwa mtu mwenye akili timamu, ina maana CHADEMA ndiyo chama cha haki na demokrasia, na CCM ni chama kinacholinda dhuluma na ufisadi. Maana kila anayepinga dhuluma wanamsema kuwa ni CHADEMA. Ikimaanisha kuwa ndani ya CCM hawataki hak wala demokrasia, na wanalinda ufisadi.