M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,026
Kama nchi kupitia Serikali yetu, ninaamini mkazo mkubwa kwa vijana wetu wanapokuwa mashuleni na vyuoni ni kuhakikisha kuwa wanajikita katika makusudi ya msingi yaliyowapeleka kwenye tassisi walizopelekwa kusoma.
Kila Mtanzania mwenye nia njema na watoto wetu (hususani wale wa kike) anao wajibu katika kuhakikisha kuwa watoto wetu hawa wanasoma katika mazingira rafiki na hatimaye waweze kufikia azma ya kupata elimu na maarifa kwa manufaa yao wenyewe, familia zao na hata taifa kwa ujumla.
Huko vyuoni kwa miaka mingi tumeshuhudia mabinti wengi wakipitia manyanyaso makubwa ya kijinsia kutokana na usichana wao tu. Wamejikuta ni helpless calves (ndama) katikati ya kundi la mbwa mwitu wenye uchu ambao badala ya kuwapa maarifa kusudiwa, wao wanataka kuwatafuna watoto wa watu masikini.
Hii imepelekea wasichana wengi ama kushindwa kumaliza masomo yao kabisa ama hata wale wanaoweza kumaliza ni ile bora liende tu lakini hawaondoki na knowledge yoyote kutokana na kuwa traumatized na unyanyasaji unaotokana na tabia chafu za hao "mafisi" huko vyuoni. Hii inasikitisha sana sana sana tena sana.
Sasa, hapa juzi tu tumemsikia na kumuona kiongozi mmoja mkubwa kabisa akiwatuma (in fact alikuwa ni kama anawaamuru) wasaidizi wake waende vyuoni UDOM & CBE eti kutafuta wake wa kuwaoa. Tafsiri yake ni moja tu kwamba hao mabinti sasa watakuwa wanakabiliana na double sword situation - yaani "mafisi" kutoka nje (ambao kiukweli ndiyo walipaswa kuwa ni kimbilio lao kwa kupeleka kilio chao in the first place) halafu na wale wa ndani (waalimu wao).
Wanabodi wenzangu niwaulize: Je, alichofanya huyu kiongozi ni sahihi kweli?
Labda ni mimi tu!