Wana JF,
Hebu tutafakari kidogo katika hili, inakuwaje kuna dini nyingi lakini zinahubiri Mungu mmoja? Tena zingine zinatufanya tusishirikiane kwa baadhi ya desturi za maisha mfano, katika vyakula, mavazi, namna ya kuabudu, mazishi nk, lakini ajabu niionayo mimi ni pale wote hawa wanapotumia pesa moja bila kubaguana! Mfano, kwanini hakuna utaratibu wa kusema hii 500/- uliyonipa ni ya kikrito ili hali mimi ni muislam/mpagani ama kinyume chake! Kwanini ufuasi wa Mungu unawafanya watu watofautiane katika imani na wakati huo wote wanafanywa kuwa wamoja katika pesa? Wenzagu mliwahi kuwaza haya? Karibuni kwa fikra njema za kutufanya kuwa wamoja.
Sorry kwa watakaokwazika kiimani!