Wamiliki wa magari madogo binafsi wanatakiwa waunde uongozi ili kufikisha kero zao kwa serikali

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,753
22,497
Nashauri wamiliki wa magari madogo binafsi waunde muundo wa uongozi ili kufikisha kero zao kwa serikali!

Mathalani kero ya kodi ya maegesho (parking fees) Hii ni moja ya tozo ya kifedhuli ambayo hutozwa na TARURA/Manispaa kwa mmiliki pasipo sababu za msingi kwasababu!

Mtu ambaye amelipia ushuru wa manunuzi bandarini na kulipia road license katika kila rita moja ya mafuta!
Road license maana yake ni kibali cha kutumia barabara pamoja na kupark katika maegesho ya barabara!
Sasa unapomchaji mtu pesa ya parking mnataka watu gari wakapaki angani? Kwanini kuna dabo kodi kwenye chombo kimoja kwa majina tofauti?

Kwanza hata hayo maegesho mnapotoza hamkuyajenga nyinyi sasa kwanini mnaleta kero kama hizi kwa wamiliki wa magari binafsi?

Kama mnataka kupata pesa za maegesho kila manispaa ijenge Parking yard ili watu wakapark huko ndiko walipie?

Lakini hii tabia ya kuvizia watu walioegesha gari pembeni mwa barabara ni uchokoraa kwa mgongo wa kimamlaka!

Wenye magari madogo undeni uongozi wa kupeleka kero zenu wasipo wasikia mnagoma mnafunga njia!
 
nagonga meza kuunga mkono. ukimani kuna mambo ya kishamba yamejazana.
Viongozi hawana ubunifu kabisa hawafai hata kukalia viti maofisni! Kodi za parking unless iwe ni miradi ya watu! Haifai kabisa kuwepo
 
Naunga mkono, miguu, kichwa na viungo vyote,

Yaani mkuu umeleta hoja bora sana

Sasa tunaanzaje?

Mimi nimelipia kifurushi cha parking cha mwezi na bado nikachajiwa hela ya kila siku na nalazimishwa kulipia na ushahidi wa risiti ninao

Yaani ni dhulma juu ya dhulma

Tufanyeje tuungane? Tupinge hii dhulma

500 mara saa 10 mara gari 100,000 tu, unajua ni shilingi ngapi?

Tena hayo ni makisio ya chini sana kwa siku moja
 
Nashauri wamiliki wa magari madogo binafsi waunde muundo wa uongozi ili kufikisha kero zao kwa serikali!

Mathalani kero ya kodi ya maegesho (parking fees) Hii ni moja ya tozo ya kifedhuli ambayo hutozwa na TARURA/Manispaa kwa mmiliki pasipo sababu za msingi kwasababu...
Wanachaji hela ya parking lakini gari yako ikipata shida kwenye hizo parking hawahusiki
 
Umeongea point sana mkuu kati ya vitu navyoshangaa Tanzania ni kulipia huo ushuru wa Kijambazi yaani ipo siku watataka ushuru kwa gari hata ukipaki nyumbani.

Ushuru unatakiwa uwepo sehemu maalumu za Mall au sehemu za maegesho ya magari sio tu mtaani harafu unakutana na ushuru wa nini wakati hizo Gari zenyewe mpaka zinaingia hapo zimelipiwa mamilioni ya kutosha na bado watu wanalipia kodi kwenye mafuta...
 
Nashauri wamiliki wa magari madogo binafsi waunde muundo wa uongozi ili kufikisha kero zao kwa serikali!

Mathalani kero ya kodi ya maegesho (parking fees) Hii ni moja ya tozo ya kifedhuli ambayo hutozwa na TARURA/Manispaa kwa mmiliki pasipo sababu za msingi kwasababu...
Hii nchi ina watu wana akili sana sijui kwa nini chawa wanaonekana sana kuliko akili hizi, anyway kutakucha tu!!!!
 
Hawa jamaa wa ajabu sana mpaka siku za sikukuu kitaifa ambapo ni mapumziko hakuna kazi lakini jamaa wanaingia mzigoni kudai pesa za maegosho !!! ukiuliza wanasema tumepewa maelekezo na mkurugenzi wa jiji ! Au parking fee ni dili la watu ??? Tutafakari
 
Nashauri wamiliki wa magari madogo binafsi waunde muundo wa uongozi ili kufikisha kero zao kwa serikali!

Mathalani kero ya kodi ya maegesho (parking fees) Hii ni moja ya tozo ya kifedhuli ambayo hutozwa na TARURA/Manispaa kwa mmiliki pasipo sababu za msingi kwasababu!

Mtu ambaye amelipia ushuru wa manunuzi bandarini na kulipia road license katika kila rita moja ya mafuta!
Road license maana yake ni kibali cha kutumia barabara pamoja na kupark katika maegesho ya barabara!
Sasa unapomchaji mtu pesa ya parking mnataka watu gari wakapaki angani? Kwanini kuna dabo kodi kwenye chombo kimoja kwa majina tofauti?

Kwanza hata hayo maegesho mnapotoza hamkuyajenga nyinyi sasa kwanini mnaleta kero kama hizi kwa wamiliki wa magari binafsi?

Kama mnataka kupata pesa za maegesho kila manispaa ijenge Parking yard ili watu wakapark huko ndiko walipie?

Lakini hii tabia ya kuvizia watu walioegesha gari pembeni mwa barabara ni uchokoraa kwa mgongo wa kimamlaka!

Wenye magari madogo undeni uongozi wa kupeleka kero zenu wasipo wasikia mnagoma mnafunga njia!
Mbona ni kawaida dunian huko
 
Kwenye hili la parking fee Kuna mambo matatu yananikera

1. Wana charge parking fee bila mwenye gari kujua na mara nyingi hawaweki kikaratasi cha bill. Yaani usipokuwa na tabia ya kuangalia kwenye ile menu huwezi kujua kama unadaiwa.

2. Sometimes wanaku charge hata kama hujapaki. Let say umesimama kumshusha mtu au abiria wako mmoja ameshuka kwenda dukani kununua kitu fulani chapa na wengine mko kwenye gari na wala gari haijazimwa.

3. La mwisho ambalo ni kero sana kwangu ndani ya muda mfupi (less than an hour) wanaweza kuku charge more than once. Yaani uko mjini unazunguka kutafuta bidhaa fulani unakuta yule wa kule kaku charge na wa huku kaku charge pia.
 
Ukosefu wa ubunifu! Wanachojua kuleta kero tu kwa wengine!
 
Back
Top Bottom