Wamasai walifikaje na kuishi Ngorongoro?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,563
14,028
Nimetembelea bonde la Ngorongoro mara kadhaa na kuona wanyama pori wengi ndani ya kama shimo hivi, inavutia sana na kushangaza. Lakini nimeona pia na makundi ya ng'ombe, punda, mbuzi na kondoo humohumo wanachumgwa na wamasai.

Naomba mtu anaefahamu atusaidie kujibu maswali haya kwaajili ya kupanua uelewa wa Wana jf.
1. Kati ya Wafugaji na wanyama nani walifika kwanza ngorongoro?

2. Kabla ya kufika Ngorongoro kuishi Wafugaji hawa wamasai walikuwa wanaishi wapi?
3. Nani aliwaruhisu Masai waishi ngorongoro pamoja na wanyama?
4. Je, waliruhusiwa kabila Moja TU la wamasai kuishi Ngorongoro na wanyama au na makabila mengine?
5. Je, Ngorongoro ya sasa Kuna Wafugaji wa kimasai TU au yapo na makabila mengine ambayo hayafugi?
6. Je, tabia na maisha ya Masai waliohamia Ngorongoro enzi hizo ya kula nyama na maziwa TU, kulala chini na nje yamebaki yaleyale mpaka sasa?
7. Sababu zikizowahamishia Ngorongoro Masai haziwezi kutumika kuwahamisha sehemu nyingine Tena Kupisha Ngorongoro na wanyama?
 
Mbona wewe hatujakuuliza hapo unapoishi ulifikaje?
Nilikuwa naishi pale Kipawa lakini nikatimuliwa nikaondoka ili kupisha ujenzi wa terminal III sasa hivi naishi kusikojulikana. Mbona Sheria haikunitetea kama inavyotaka kutetea Ngorongoro?
 
Back
Top Bottom