Wamasai ni watu poa sana!

kikokoteo

JF-Expert Member
May 11, 2024
250
365
Nilibahatka kuoa binti wa kimasai, nilikuwa sina maisha napitia changamoto ya maisha lakini yeye wala hakunikimbia. Kitu alichoniambia nimtafutie shilingi elfu 35,000/= ya kufanya ujasiriamali ya kuendesha biashara ya mboga mboga kwenye minada ya wamaasai.

Huwezi amini ndani ya miaka 2 kanipga gepu ya maendeleo pakubwa, sasa hivi anauza Mavazi ya kimasai huko mnadani. Kiwanja tumenunua kwa pamoja ila yeye ndiye kachangia pakubwa.

Mwez wa kumi na mbili mama mkwe anakuja kumshka mtot yaan mjukuu wake sasa mke amenitonya nitafute pesa ya sherehe kama milioni 3 maana yeye kaambiwa na mama yake watakuja na milioni 14 kwa wamasai ndiyo desturi yao wanaita mbesi mama kwenda kwa mtoto wake wa kike kumsalimia duh! Kweli ya Mungu mengi.
 
Embesi ni shughuli ya kumsupport mtu katika jambo lake. Mfano, kupata mtoto, sherehe yeyote, au matatizo.

Mkweo naye huwa ana kikundi cha umoja wao ambao wanasaidiana. Sasa imefika zamu yake, naye kapata jambo. Mwanae kajifungua, wanakuja kumsalimia.

Sasa watakapokuja watafika na vitu kibao maalum haswa kwa mtoto na mzazi wake. Vyakula, nguo, hela, nk

Sasa wakijaga wewe uttagharamikia hela ya chakula na vinywaji tu. Uhakikishe kuwa wanakula na kunywa na kusaza.

Utapata zaidi ya ulichokitumia. Nina uhakika.

Wamasai ni watu wavumilivu mno. Haswa wale ambao dunia haijawameza. Watii na wana adabu mno. Huvumilia katika mengi.

Nakutakia kila la kheri.
 
Nilibahatka kuoa binti wa kimasai, nilikuwa sina maisha napitia changamoto ya maisha lakini yeye wala hakunikimbia. Kitu alichoniambia nimtafutie shilingi elfu 35,000/= ya kufanya ujasiriamali ya kuendesha biashara ya mboga mboga kwenye minada ya wamaasai.

Huwezi amini ndani ya miaka 2 kanipga gepu ya maendeleo pakubwa, sasa hivi anauza Mavazi ya kimasai huko mnadani. Kiwanja tumenunua kwa pamoja ila yeye ndiye kachangia pakubwa.

Mwez wa kumi na mbili mama mkwe anakuja kumshka mtot yaan mjukuu wake sasa mke amenitonya nitafute pesa ya sherehe kama milioni 3 maana yeye kaambiwa na mama yake watakuja na milioni 14 kwa wamasai ndiyo desturi yao wanaita mbesi mama kwenda kwa mtoto wake wa kike kumsalimia duh! Kweli ya Mungu mengi.
Hawafai kuongoza nchi!
Hawajuagi democrasia wanachojua n ubabe kifupi watusi na wamasai siyo kabisa kwene uongozi
 
Ila kweli, ukiona zimepungua, oa aliyekuzidi akili.
Jana nilikuwa na binamu yangu kwenye party, yeye ni mlevi na mpenda starehe. Ni wale akitoka Ijumaa asubuhi kwenda kwenye ujasiriamali kwake anarudi Jumatatu usiku. Ile Ijumaa anaunga kazini hadi starehe, anaibuka asubuhi starehe anaenda kutafuta, hivyohivyo mpaka akirudi Jumatatu usiku ndio analala. Kwahiyo alikuwa anakaa mchafu na ananuka pombe.

Sasa jana nikashangaa mbona ametoka uzee, kanawiri, macho yamepungua wekundu na hajavimba uso. Kumbe ameoa sogea tuishi kaacha kulala viwanja na kunywa supu ya mapupu. Mke yuko strict hakuna kulala nje wala kurudi umelewa.

Binamu hadi jana tukazungumzia kilimo na viwanja, na kusafirisha mikoani. Akataja hela ambazo kabla hajawahi taja, na manunuzi ambayo hakuwa anafanya. Nikagundua tu hizi akili ni mchango wa mke wake.
 
Back
Top Bottom