NadeOj
JF-Expert Member
- Mar 25, 2024
- 454
- 857
Kama umewahi kujiuliza ukifa unaenda wapi au inakuaje, hili ni swali ambalo linakosa majibu rasmi lakini wanasayansi wamejaribu kulifuatilia kwa ukaribu na kulifanyia utafiti kwa miaka mingi.
Utafiti wao ulijikita katika watu ambao walinusurika katika kifo kwenye majanga mfano ajali, kuzama ndani ya maji, mshituko wa moyo na wagonjwa waliofikia hali mbaya zaidi karibu na kufa.
Katika tafiti hizi tangu miaka ya 1975 walihojiwa zaidi ya watu 200 ambao walikua ni manusura walio kichungulia kifo.
Katika vitu ambavyo walivieleza manusura hao, kuna baadhi ya vitu takriban kila manusura alielezea kua alikipitia wakati akikabiliwa na hatari ya kufa,
Wanasayansi wakachambua mambo hayo ambayo takriban kila manusura alielezea kuyapitia wakati huo na kuyaita "Near Death Experience" ( N D E )
Near Death Experience - haya ndo mambo ambayo takriban kila moja hupitia dakika chache kabla ya kufa
1. Out-of-body experiences (O B E) / Kujihisi upo nje ya mwili
watu walio pitia NDE wanaeleza kua kuna muda walikua wanajiona nje ya mwili, na kuwaona jinsi madaktari au manesi walivyokua wakiuhangaikia mwili na hata kusikia yanayoongelewa, pia wengi wanasimulia matukio yaliyokua yanatokea hapo na watu waliokwepo muda huo kwa usahihi mkubwa kabisa.
2. Kupita kwenye tunnel
kitu kingine kinachoelezewa na watu waliopitia NDE ni kupita kwenye tunnel ( kama bomba ) yenye giza ambapo upande wa mbele kunaonekana mwanga ambapo wanapita kuuelekea mwanga
huku tunnel ikionekana kama haiishi lakini mwanga wanaouona kwa mbali unawaletea hisia ya amani na upendo.
3. Kukutana na watu
wengine wanaeleza kua walikutana na wapendwa wao ambao walishakufa tayari, wengine pia wakieleza kukutana na watu wa kiimani (spiritual figures) ambapo hao watu wana waongoza na kuwatoa wasiwasi.
4. Kuhisi amani na upendo (unconditional love)
wengi wanaeleza kuhisi amani na upendo wa hali ya juu sana na kujihisi kuwa na muunganiko na kila kitu kilichowazunguka.
5. Kuona matukio ya maisha
takriban wote waliopitia NDE wanaeleza kuona matukio mbalimbali waliyofanya katika maisha yao na jinsi yalivyo waathiri wengine na wenyewe binafsi kwa uzuri au ubaya.
6. Chaguo la kurudi katika mwili
karibu watu wote waliopitia NDE Wanaripoti kua kuna sehemu walifika wakapewa chaguo la kuendelea mbele au kurudi ambapo pia inaambatana na ufahamu kua muda wao wa kuishi duniani bado haujaisha kwahiyo wanatakiwa kurudi ili kukamilisha jambo fulani.
pia watu waliopitia Near death experiences (NDE) wanaonekana kuathiriwa na hali hii
ambapo wengi waao hubadika kabisa katika mtindo wao wa maisha baada ya kunusurika na wote huonyesha mabadiliko ya kufanana kwenye Maisha yao kama vile:
1. Kupungua kwa hali ya kuogopa kufa
watu waliopitia NDE wanakua hawana hali ya kuogopa kifo tofauti na watu ambao hawajapitia NDE
2. Wanaongezekewa na hali ya kujiona wa thamani
wengi hujiona kua wamekuja duniani kwa kusudi fulani au walinusurika kwa kusudi fulani
3. Hali ya kujali watu inaongezeka
Takriban watu wote waliopitia NDE wanakua wanathamini sana maisha ya watu wengine na kujihusisha zaidi kwenye shuguli za kijamii na kusaidia wengine kuliko walivyokua kabla ya kupitia NDE.
Kama na wewe au mtu unaemjua amewahi kupitia Near Death Experience (NDE) tujuze