Wadau naomba nipewe muongozo wa hawa wakuu waliotumbuliwa (Kusimamishwa kazi) sipendi kutumia sana hilo neno kutumbuliwa kwasababu halina maana kwangu kwa jinsi linavyoshadidiwa.
Nirudi kwenye mada ninachotaka kujuzwa ni je Wao watumbuliwa bado wanendelea kutumia hizo Passport za kidiplomasia na kama sivyo mbona sijasikia popote wakikabidhi hizo hati za kusafiria kwa vyombo husika na kupewa hizi za sisi walalahoi. au kusimimishwa kwao kazi hakuuondoi udiplomasia wao.