Teknocrat
JF-Expert Member
- Oct 20, 2018
- 4,578
- 10,423
Ni miaka takbiran mitatu sasa tokea nichomwe chanjo ya kuzuia maabukizi ya COVID (UVIKO).
Mimi nilichoma chanjo ya Pfizer Biontech, na zilikuwa dozi mbili zikipishasha wiki 6 mpaka miezi miwili.
Na mpaka sasa nadunda na miezi kadhaa iliyopita tulimkaribisha mgeni mpya wa dunia hii.
Zilikuwepo pilika nyingi sana za njama potofu (conspiracy theories) nyingi duniani kuhusu kuanzia uwepo wa ugonjwa wenyewe wa COVID na kuendelea mpaka kwenye chanjo yenyewe ya COVID
Waliibuka wataalamu wa kweli hasa kielimu kila pande za dunia kupinga na kusambaza habari potofu kuhusu maambukizi ya ugonjwa COVID na chanjo yake.
Walituaminisha njama potofu kedekede kuhusu maigizo yanayofanywa mahospitalini kuhudumia wagonjwa wa COVID ni kama sinema zinachezwa na kutangazwa na vyombo vya habari ambavyo vyote viko kwenye hii njama ya kuhadaa walimwengu.
Pia walijitokeza wataalamu wa utafiti wa kinga za kibaologia kwenye kila mitandao ya jamii, wakitutahadharisha athari za kinga ya COVID kuwa ni njama ya kuturaibu tuzoee dozi ya COVID kama uraibu wa madawa ya kulevya na pia kutunga na kuchombezea kila athari zilizotokana na vifo vya ghafla kwa wachomwaji wa kinga ya COVID ni njama ya kupunguza idadi ya watu duniani.
Pia kulitokea wale watafuta fursa kwenye mitandao ya kijamii, walioneza njama mfu ya kuwa kinga ya COVID ina chembechembe za kielectroniki(CHIP) ambazo ni mpango maalumu wa kusambza mlingonti ya teknologia ya 5G, ambazo zingetumika kuziendesha hizo CHIP zilizopandikizwa kwa njia ya chanjo na kuwa kila aliyechoma chanjo atakuwa anapokea maagizo kimtandao na ya kuteleza kama MSUKULE.
Haya tunahitaji mrejesho kwa wale waatalum waaliojulikana kama spin doctors.
cc Mathanzua, Let me get this straight about the COVID-19 vaccine