Waliomuua yule mtoto albino wahasiwe haraka sana, hawana sifa ya kuitwa binadamu

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
576
2,400
Huyu mtoto hadi mmekatisha uhai wake amewakosea nini jamani, hili jambo kila ninapofanya shughuli zangu linanijia, nimevaa uhusika kuwa yule ni binti yangu amefanyiwa unyama ule, niko katika hali gani.

Kweli nyie mliofanya unyama na ukatili kiasi hicho mnastahili kuwepo duniani kweli?

Huyu mtoto amewakosea nini nyie, yaan mmemuwinda kama mnyama kweli halafu mmekutwa na baadhi ya viungo vyake jamani.Aisee.

Hao waliokamatwa kwanza wahasiwe hata kama upelelezi unaendelea lakin wahasiwe kwanza watie akili, kuwapeleka mahabusu washenzi hao ni kuwapendelea tu.

Serikali iendelee kufanya msako nyumba hadi nyumba kukomesha ukatili huo.

Pia soma:
 
Kenya wanafanya sana Investigative journalism. Watu kama kina John Alan Namu, Mohamed Jicho Pevu, Purity Mwambya n the likes. Hawa wangekuwa wameshawataja wahusika hasa wa hii biashara at least ingepunguza hii aibu. Tanzania tunapata aibu Sana kimataifa kwenye hili. To some extent nahisi kama serikali imelishindwa.
 
Acha hasira za kijinga. Bado wana nafasi ya kubadilika na wakawa watu wema. Wapewe adhabu zinazostahiki lkn zisikiuke misingi ya kiutu.

Kosa halitibiwi kwa kosa.
Sorry to say this, ila wewe Una makamasi kichwani.
 
Hawa wangekuwa wameshawataja wahusika hasa wa hii biashara
Huwajui wahusika wa hii biashara? Mbona inajullikana kitambo sana!

Wanasiasa wa kabila la "inhiiii!!!" Hawa ndiyo wanaochochea biashara hii na ndiyo wateja wakubwa kila ukikaribua uchaguzi.
 
Elimu muhimu sana

Kwa hiyo wamegawana bilioni ngapi?

Upuuzi tu na hizi imani za kingese

Halafu utawakuta hao wauaji wakijua unabet utasikia betting ni dhambi , sawa bora nibet na sio kutafuta njia za mkato za kingese
 
Kenya wanafanya sana Investigative journalism. Watu kama kina John Alan Namu, Mohamed Jicho Pevu, Purity Mwambya n the likes. Hawa wangekuwa wameshawataja wahusika hasa wa hii biashara at least ingepunguza hii aibu. Tanzania tunapata aibu Sana kimataifa kwenye hili. To some extent nahisi kama serikali imelishindwa.
Ishawahi kufanyika hii na aljazeera nadhani ilikuwa shinyanga na journalist mmoja anaitwa anas ni mghana nadhani akishirikiana na mwandishi wa bongo jina silikumbuki walienda kwa mganga na camera za siri mganga akaawambia walete viungo vya albino jamaa wakaleta mkono wa albino bandia ila ukiungalia kama wenyewe mganga akapagawa wakamtaitisha na polisi kwani pia alikutwa na viungo ambavyo vimesagwa vimekuwa unga wanaviita vingira, aliviweka wenye makopo
 
Wanastahiki adhabu kali kulingana na sheria za jamuhuri ya muungano wa Tanzania
 
Hahaha nchi hii yenye tatizo la nguvu za kiume, halafu u wa hasi tena? Unaweza kuta walitaka viungo wapate dawa ya nguvu za kiume na dawa bado hawajapata.
 
Back
Top Bottom