Waliomtandika bakora Mwanamke huko Wilaya ya Rorya wakamatwa

Jeshi letu bhana mambo ya vifo kule Ruvu hatujaskia mtu kakamatwa, mtu akitandikwa viboko tayari watuhumiwa wameshakamatwa, Ahsanteni Polisi Tanzania.
 
Kitendo cha kumtandika yule mama kimeonekana kweli kuwa ni ukatili sana, na kamwe haifai kuungwa mkono kwa vitendo vya namna hiyo!
..tatizo lipo bado kwa hawa wanaoamini hizi imani za kishirikina, kama maelezo yanavyusema kuwa alimuambia mama yake kuwa atamuua kwa uchawi bila shaka hiyo ndiyo iliyozua taharuki na hatimaye ikaamuriwa apigwe bakora!
Busara zaidi ingehitajika kutatua huo mgogoro, lakini pengine ilionekana huyo mama ni mtu hatari ikapelekea maamuzi kama hayo kutolewa!!
 
nimeamini mkono wa serikali cyo mfupi .pongezi kwa wote mlioshiki kwa namna moja ama nyingine hao watuhumiwa kukamatwa hili litasaidia kupunguza unyanyasaji wa kijinsia
 
Niliumia sana, hasa ukivaa uhusika kuwa anaepigwa vile ni mama yako......
Ni kweli aisee sijui watu huwa wanatumwa na waganga wa jaji!

Binadamu anafanya mambo ya kijinga sana, kuna matukio mengine shetani hujifunzia kwa binadamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…