Maghayo
JF-Expert Member
- Oct 5, 2014
- 14,992
- 33,140
Mzuka wanajamvi!
Genge la vijana waliokulia udogoni na kiungo wa zamani wa Manchester united na Sasa mchezaji wa Juventus Italia wanadai fadhila ya kulipwa hela na Paul Pogba kwa nguvu.
Marafiki hao wa Pogba Toka udogoni waliokulia viungani mjini Paris wanadai Pogba kawasahau. Wamekumbusha Pogba wamekuwa wakimlinda bila yeye kujua tangu alipoanza kupata umaarufu na kukamata hela ndefu.
April mwaka huu yasemekana walimteka Pogba na kumpeleka ghetto la rafiki yao chini ya ulinzi mkali wa bunduki na kumkalisha chini na kumkumbushia jinsi walivyokua pamoja toka udogoni na alivyowasahau.
Na kumuonya na kumtishia maisha endapo asipowasaidia. Na pia wame mblackmail Pogba Euro million 13. Asipowapa hizo hela wataweka hadharani matukio na mambo ya ajabu Pogba aliyokuwa akifanya zamani.
Pogba mwenyewe anajitetea hajawahi kuwasahau masela zake. Kila mara walipohitaji msaada wa pesa aliwapa. Anasema kuna wengine hadi aliwakaribisha kuishi nao kwake alipokuwa Manchester.
Lakini ikabidi kuwafukuza na kukata urafiki na mawasiliano baada ya mmoja wao kumuibia kadi ya benki na kutumia kutoa hela kiasi cha paundi za uingereza laki mbili.