Waliofutiwa Matokeo ya kidato cha 4, 2022 wapewa idhini ya Kurudia Mtihani

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,126
1,922
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa idhini kwa wanafunzi 337 waliofutiwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2022 na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kurudia mtihani huo.

Wanafunzi hao walifutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwemo udanyanyifu na wakaomba kupewa nafasi ya kurudia mtihani huo.

Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda amesema jijini Dodoma kuwa ruhusa hiyo ni kwa wanafunzi wote waliofutiwa matokeo wakiwemo wanafunzi wanne waliofutiwa kwa kuandika matusi.

"Tungesema hawa wanafunzi warudie mitihani na wenzao wa kidato cha nne kwa utaratibu wa kawaida kama ilivyozoeleka serikali ingepata hasara zaidi ya Sh bilioni moja ila kwa utaratibu huu wa kuomba wenyewe kama na kufanya mtihani huo pamoja na wenzao wanaofanya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu kwa utaratibu utakaowekwa na NECTA basi itasaidia sana kupunguza gharama," amesema Prof. Mkenda.

Utaratibu wa kurudia mitihani kwa wanafunzi hao utakwenda sambamba na mitihani ya kidato cha sita ambao unatarajiwa kuanza Mei 2, 2023, hivyo watawekewa utaratibu wa kuchanganyika pamoja wakati wa kurudia mitihani hiyo.

Pia amewataka watanzania kukemea kwa pamoja matukio ya wizi wa mitihani kwani inafundisha watoto udanganyifu na kuondoa weledi na kuwanyima haki watahiniwa ambao hawajashiriki katika wizi huo.

Chanzo: Habari Leo
 
Hapo kwenye gharama ya bilioni moja bado sijaelewa vizuri.

Ina maana mtihani wa watu 330 unagharimu bilioni moja!

Kwamba mtihani wa mwanafunzi mmoja kuanzia kutungwa, kusafirishwa, kusimamiwa, kusahihishwa, kupangwa matokeo n.k ni kati ya milioni tau (3,000,000)

Naomba kueleweshwa
 
Hapo kwenye gharama ya bilioni moja bado sijaelewa vizuri.

Ina maana mtihani wa watu 330 unagharimu bilioni moja...
Mimi ndio Ndio Sijasoma hesab vzr...

1,000,000,000/330 = 3,030,303..

Ambapo ni almost 3M @ Each..

Bora walioiba walikua na nia ya kufaulu kuliko hao mazuzu walioandika matusi, hao hata huo msamaha hawewezi kuufurahia.
 
Athari za kurudia mtihani mara nyingi majibu yake huwa hasi kwa sababu morali ya kusoma kwa bidii hushuka. Kama mtihani wa awali ulikuwa ufaulu wa pili unafeli, na kinyume chake pia, bora kinyume chake. Kwa ujumla mitihani ya kurudia ni bahati nasibu kufaulu na ni pata potea
 
Athari za kurudia mtihani mara nyingi majibu yake huwa hasi kwa sababu morali ya kusoma kwa bidii hushuka. Kama mtihani wa awali ulikuwa ufaulu wa pili unafeli, na kinyume chake pia, bora kinyume chake. Kwa ujumla mitihani ya kurudia ni bahati nasibu kufaulu na ni pata potea
Cha muhimu wapate vyeti vya form four kwanza
 
Back
Top Bottom