Waliofungwa jela maisha ni matokeo ya Uchawa. Anayekutuma hatakuwepo siku ya madhira juu yako

Bush Dokta

JF-Expert Member
Apr 11, 2023
20,275
37,421
Ndani ya Taifa letu ni wazi sasa Tunu ya Vijana imekuwa ni Uchawa.

Ili utoboe maisha lazima uwe chawa wa kisiasa au wa namna nyingine pia.
Waliofungwa miaka ya maisha Jela ni chawa ambao awali zilivuma kuwa walitumwa.

Ukitazama nyuso za wale vijana zilo Innocent kabisa. Huwezi kufikiria kuwa watafanya vitendo vya kinyama namna ile.

- Nyundo na wenzake wakutwa na hatia, wahukumiwa kifungo cha Maisha Jela

Hata huku kwenye siasa kumezuka chawa wa hatari sana. Chawa ambaye akitumwa kamuue fulani anakusaka na mapanga hata bila kujiuliza kwanini afanye hivyo.

Kilichotokea kiwe fundisho kwa chawa wenye mihemko wakidhani watalindwa na anayewatuma.

Serikali ikiamua kukufata weww Chawa hata anayekutuma atakugeuka na kukukimbia. Utabaki wewe na familia yako tu.

Be warned.
 
Na bahati nzuri kwa sheria zetu anayetumwa kufanya unyama ndiye anaadhibiwa.

1. Askari waliotwa na Abdallah Zombe kuwaua wafanyabiashara waliadhibiwa. Askari aliyefyatua risasi alihukumiwa kifungo cha maisha.

2. Jambazi aliyetumwa na mke wa bilionea Msuya kwenda kumuua dada wa bilionea Msuya ndiye aliyehukumiwa kifungo cha maisha.

3. Vijana waliotumwa na afande kwenda kubaka ndiyo wamehukiwa kifungo cha maisha.

4. Vijana wanaotumwa kwenda kuteka na kuua ndiyo watahukumiwa kifungo cha maisha jela.
 
Na bahati nzuri kwa sheria zetu anayetumwa kufanya unyama ndiye anaadhibiwa.

1. Askari waliotwa na Abdallah Zombe kuwaua wafanyabiashara waliadhibiwa. Askari aliyefyatua risasi alihukumiwa kifungo cha maisha...
Hili liwe funzo kubwa
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Back
Top Bottom