Nusra Shaaban
New Member
- Oct 8, 2024
- 2
- 1
Na Nusra Shaaban
Walimu wapya walioajiriwa katika Wilaya ya Mjini wametakiwa kuzingatia maadili ya taaluma, kuwa wavumilivu, na kuwa na moyo wa kujituma ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.
Akizungumza katika semina ya kuwapa nasaha za kitaaluma iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Afisi ya Elimu Wilaya ya Mjini Zanzibar, Afisa Elimu wa Wilaya ya Mjini, Hassan Abbass Hassan alisema kuwa semina hiyo inalenga kuwaandaa walimu wapya kwa majukumu mapya waliyopewa katika Skuli mbalimbali za Wilaya hiyo.
"Walimu ni nguzo muhimu katika maendeleo ya jamii yoyote. Tunawategemea kama walezi wa kizazi kijacho, hivyo nidhamu na bidii ni nguzo muhimu," alisema.
Maafisa wengine wa elimu, akiwemo Afisa Taaluma Sekondari Wahida Haidar Hasham, walitoa mwongozo kuhusu mbinu bora za ufundishaji, jinsi ya kushughulikia changamoto za wanafunzi, na umuhimu wa kushirikiana na wazazi katika kuboresha elimu.
Walimu hao walisisitizwa pia kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma ili kuepuka matatizo kazini.
Mkuu wa Ukaguzi wa Elimu wa Mkoa wa Mjini, Tatu Himidi Khamis, aliwataka walimu hao kuwa na moyo wa uzalendo, nidhamu, na bidii katika kutekeleza majukumu yao ya kufundisha na kulea wanafunzi.
Mkaguzi huyo alisisitiza kuwa taaluma ya ualimu ni msingi wa maendeleo ya taifa, hivyo inahitaji uadilifu na utayari wa kufanya kazi kwa weledi.
"Walimu ni walezi wa kizazi kijacho. Taifa linawategemea katika kulea na kuandaa viongozi wa kesho. Hivyo, ni muhimu kufanya kazi kwa bidii, kuwa wavumilivu na kuwa mfano wa kuigwa kwa wanafunzi wenu," alisema.
Aliongeza kuwa ofisi yake itaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kuhakikisha kuwa walimu wanafuata miongozo ya elimu na kwamba changamoto wanazokutana nazo zinashughulikiwa kwa wakati.
Baadhi ya walimu wapya walieleza furaha yao kwa nafasi ya kufundisha na kuahidi kufanya kazi kwa weledi na kujituma.
"Tunashukuru kwa kupitia semina hii tumepata mwanga kuhusu majukumu yetu.
Tumehamasika kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya wanafunzi wetu," alisema mmoja wa walimu wapya, Thumayya Said Abdallah, Mwalimu wa Maandalizi Skuli ya Haile Salathi.
Ahmada Khamis Maalim, mwalimu wa Sekondari Skuli ya Hurumzi, alisema semina hiyo imemfungua macho kuhusu majukumu yake kama mwalimu na ana ari kubwa ya kuwalea wanafunzi katika misingi bora ya elimu na maadili.
Semina hiyo ilijumuisha walimu wapya wapatao 75 kutoka Wilaya ya Mjini, wakiwemo walimu wa maandalizi, walimu wa maktaba, walimu wa msingi na Sekondari itasaidia kuboresha matokeo ya elimu katika Wilaya hiyo.