Walimu wa shule za msingi mna shida gani?

mchuuzi wakileo

New Member
Feb 20, 2025
1
0
Walimu wa shule ya msingi tulizeni vichwa mnapokuwa mnafanya usajili wa watoto kwenye mifumo ya serikali. Wakati wa usajili mathalan Darasa la kwanza au darasa la nne huwa mnatuagiza tulete vyeti vya kuzaliwa vya watoto ili kuepusha mpishano wa majina au herefu kwani mtoto anaposajiliwa darasa la nne majina hayo ndio hutumika Mpaka darasa la saba mpaka secondary na huwez kubadilisha tena.

Hapa ninapoandika watoto wa kidato cha pili wanafanya uhakiki wa majina kwa ajili ya mtihani wa taifa cha kushangaza jina baba na babu la mtoto wa rafiki yangu alotoka nalo shule ya msingi yamekutwa yameongezwa herufi mfano jina la baba la mtoto: ATHUMAN wao wameandika ATHUMANI kimepelekwa cheti cha kuzaliwa cha mtoto ambacho ndicho kilichotumika Wakati wa shule ya msingi kinasoma ATHUMAN, cheti cha baba nacho kinasoma hivyohivyo ATHUMAN Shule imemwambia mzazi aende kubadilisha cheti cha kuzaliwa cha mtoto kwani majina yaliyopo shule (kwenye mfumo) hayawezi kubadilishwa. Rafiki yangu ananiambia Wazazi ni wengi mno waloitwa kubadilisha vyeti vya watoto wao.

Ndugu walimu tunajua mna kazi nyingi hapo shuleni lakini nyie ni wasomi haiwezekani unapewa kabisa cheti cha mtoto Wakati wa usajili na bado mnaongeza/kupunguza herufi kwenye majina ya watoto. Mtoto huyu anaebadilisha majina hamuoni mnaenda kumsababishia matatizo mengine huko mbeleni hasa pale itakapotokea cheti cha mzazi na yeye muhusika vinaitajika kwa pamoja?

Mfano kwenye kuomba passport ya kusafiria?
 
Hili la kuongeza herufu au kuandika jina isivyo lipo sana tu kwa walimu wenye ufahamu mdogo wa kuandika majina ya wanafunzi kwa mujibu wa vyeti vyao vya kuzaliwa. Hata wazazi wa kike waliotengana na waume zao hukosea herufu za jina la baba wakati wa kuandikishwa mtoto. Unakuta mtoto anaitwa IRENE SIMON lakini mama anaenda kutamka AIRINI SAIMONI na muandikaji naye anaandika hivyo hivyo kimakosa. Ni vema walimu wakahakiki herufi za majina ya wanafunzi kabla hawajaingiza kwenye kompyuta na kutuma huko wizarani/halmashauri/NECTA
 
Back
Top Bottom