Shanily
JF-Expert Member
- Nov 4, 2024
- 768
- 1,544
Binafsi sio Mwalimu kwa taaluma lakini Huwa nafundisha wanafunzi Masomo ya ziada baadhi ya nyakati.
Katika wanafunzi nilonao wengi hawajui matumizi sahihi ya herufi na matamshi yake.
Mtu yupo darasa la 4 , la 5 na kuendelea , unajiuliza inamaana shuleni hawafundishwi na walimu wa kiswahili!?.
Walimu wenyewe hawajui matumizi na matamshi ya hizo herufi!?.
Kama wanajua kwanini hawachukui hatua kipindi mwanafunzi yupo awali , darasa la kwanza ili tatizo lisiwe kubwa!?.
Wakisahihisha mitihani hawaoni hayo makosa!?.
Nakumbuka zamani wakati nipo shule ya msingi, mwalimu wa kiswahili alikuwa mkali haswa, ukiandika herufi sio katika sentensi ujue atakupa kosa swali zima, hiyo ilitusaidia sana kukariri matamshi ya herufi na uandishi wake.
Walimu wa sasa mbona mnatuangusha!. Kiswahili kinaharibiwa mikononi mwenu!.
Unakuta mwanafunzi anaandika:
Chakura, salasini, laha, fezeha, zulma, amsini, ishilini.
Hapo bado hajazingatia alama za uandishi , yaani anaandika ilimradi kaandika na mwalimu anaona sawa hakosoi.
Tumewakabidhi jukumu la kukienzi na kukitunza kiswahili chetu, fanyeni kazi yenu kwa umahiri.