State Propaganda
JF-Expert Member
- Apr 25, 2024
- 479
- 1,194
Mimi na familia yangu leo ifikapo saa mbili kamili usiku tutakuwa sebuleni tukiangalia makala maalum iliyoandaliwa na kitengo cha utafiti wa habari cha Al Jazeera (Al Jazeera Investigation Unit) kama kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kuanza kwa vita baina ya Palestina na israeli.
Katika makala hiyo iliyoandaliwa na waandishi nguli kutoka chombo hicho cha habari chenye kuaminika kimataifa, wameanika madhila na uhalifu wa kivita ulifanywa na jeshi la IDF katika mauaji ya halaiki huko Palestina, ambayo ni kielelezo tosha cha ushahidi utakaoweza kutumika katika keshi zilizofunguliwa katika Mahakama ya Kimataifa (ICJ) dhidi ya Netanyau pamoja na serikali yake kwa ujumla.
Unaambiwa masaa machache tu tokea documentary hiyo ilipoachiwa hewani leo hii, tayari imeshaanza kukumbana na ukosoaji mkali kutoka vyombo vya habari vya kizayuni ambvyo vinadai makala hiyo imejaa ushahidi dhaifu na pia inajaribu kuudangnya ulimwengu juu ya kile kilichotokea tangu kuanza kwa mzozo huo.
Waswahili waasema kizuri kula na wenzako, hivyo nikaona niwaletee 🔗 link ya makala hiyo hapa.👇👇
View: https://twitter.com/AJIunit/status/1841885939791999043?t=loxG_ksJ9S7z9192mTtwPA&s=19
Muwe na jioni njema.