Strong ladg
Member
- Jul 15, 2021
- 50
- 136
Wakuu wa Majeshi kutoka nchi za Niger, Mali na Burkina Faso zinazounda umoja wa nchi za Sahel ( AES ) wamekutana na kufanya kikao nchini Niger jana tarehe 3 Disemba 2024.
Wakuu hao wa majeshi walifanya tathmini ya mwenendo wa mapamabano dhidi ya magaidi wanaozisumbua nchi zote tatú.
Baada ya kikao hicho, walikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Niger Brigedia Jenerali Abdul Rahman Tchiani.
Wakuu hao wa majeshi watatakiwa kuwasilisha ripoti ya kikao chao kwa Rais wa Mali Jenerali Assimi Goita ambaye kwa sasa anashikilia kiti cha urais wa umoja wa nchi za Sahel.
Tangu kuchukua madaraka kwa njia ya mapinduzi, wakuu wa nchi za Sahel wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na magaidi dhidi ya raia na wamefanikiwa kuwaondoa wanajeshi wa Ufaransa waliokuwa wamekaa kwenye nchi zao kwa miaka mingi.
Pia wamefanikiwa kuyafanyia marekebisho makubwa majeshi yao kwa kununua silaha na vifaa vipya vya kijeshi kutoka kwa washirika wengine mfano Uturuki. Hii ni baada ya kuvunja mikataba ya "uhuru" iliyokuwa inazilamisha nchi zilizotawaliwa na Ufaransa kununua silaha kutoka Ufaransa tu na si vinginevyo.
CHANZO/ SOURCE: Shirika la habari la NIger (RTN)