Wakulima wa miwa Kilombero wampinga Luhaga Mpina

ILISACHA

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
2,144
3,927
Wakulima wa Miwa katika Bonde la Mto Kilombero Mkoani Morogoro wamekanusha taarifa zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina na baadhi watu waliodanganya kuwa ni wawakilishi wa wakulima na kudai bei ya miwa imeporomoka na hawalipwi fedha zao kwa wakati.

Hii ngoma amini usiamini maelekezo tayari yashatolewa kwa wakulima.

Mi naamini bodi ya sukari haitomkana Mpina.

Wakizungumza na waandishi wa habari wilayani Kilombero viongozi wa umoja wa vyama vya wakulima pamoja na baadhi ya wakulima wanaounda vyama 17 vya ushirika (AMCOS), wamekanusha taarifa hizo wakidai kuwa ni uzushi na upotoshaji unaofanywa kwa maslahi ya kisiasa.

“Hakujawahi kutokea bei ya miwa kushuka kwani tangu tuanze kuuza miwa msimu huu tumeuza kwa bei ya laki moja na elfu nane (108,000) – tofauti na hizi taarifa za uongo zinazosambaa”

Aidha wakulima hao wamedai kuwa hakujawahi tutokea ucheleweshwaji wa muda mrefu wa malipo kwa wakulima kutoka kwenye kiwanda cha kuzalisha miwa na badala yake malipo yalichelewa kwa siku mbili tu kutokana na mifumo mipya iliyowekwa kiwandani hapo ambapo walitakiwa kulipwa tarehe 15 na badala yake walilipwa tarehe 17.

Wakulima hao wamesisitiza kwamba hakuna athari zozote zilizowapata kufuatia uamuzi wa serikali kutoa vibali vya kuagiza sukari nje kupunguza ongozeko la bei ya bidhaa hiyo ili kuleta ahueni kwa wananchi.

Vilevile wakulima hao wamesema kuwa vyama vyao vina ushirikiano mzuri na kiwanda cha sukari Kilombero na wanayo matumaini makubwa ya mageuzi ya zao hilo, kwa kuwa kiwanda hicho kinalenga kufanya upanuzi mkubwa utakaopelekea wakulima kuuza miwa kwa wingi zaidi.

Pia soma
 
Wenye miwa yao wamekuja juu, na wanasema Lihaga Mpina ni muongo wa kutupwa, bei ya miwa haijashuka, na viwanda vinainunua kwa kasi kubwa.

Yaani Mpina haongelei bei ya pamba jimboni kwake, anahangaika na miwa inayolimwa kilometa zaidi ya 1000 kutoka kwenye jimbo lake
Screenshot_20240801-085424.jpg
Screenshot_20240801-085438.jpg
 
ADUI YAKO HATOKI MBALI NAWE!
WASALITI WALIKUWEPO, WAPO NA WATAENDELEA KUWEPO.
 
Wakulima wa Miwa katika Bonde la Mto Kilombero Mkoani Morogoro wamekanusha taarifa zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina na baadhi watu waliodanganya kuwa ni wawakilishi wa wakulima na kudai bei ya miwa imeporomoka na hawalipwi fedha zao kwa wakati.

Hii ngoma amini usiamini maelekezo tayari yashatolewa kwa wakulima.

Mi naamini bodi ya sukari haitomkana Mpina.

Wakulima wa Miwa katika Bonde la Mto Kilombero Mkoani Morogoro wamekanusha taarifa zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina na baadhi watu waliodanganya kuwa ni wawakilishi wa wakulima na kudai bei ya miwa imeporomoka na hawalipwi fedha zao kwa wakati.

Wakizungumza na waandishi wa habari wilayani Kilombero viongozi wa umoja wa vyama vya wakulima pamoja na baadhi ya wakulima wanaounda vyama 17 vya ushirika (AMCOS), wamekanusha taarifa hizo wakidai kuwa ni uzushi na upotoshaji unaofanywa kwa maslahi ya kisiasa.

“Hakujawahi kutokea bei ya miwa kushuka kwani tangu tuanze kuuza miwa msimu huu tumeuza kwa bei ya laki moja na elfu nane (108,000) – tofauti na hizi taarifa za uongo zinazosambaa”

Aidha wakulima hao wamedai kuwa hakujawahi tutokea ucheleweshwaji wa muda mrefu wa malipo kwa wakulima kutoka kwenye kiwanda cha kuzalisha miwa na badala yake malipo yalichelewa kwa siku mbili tu kutokana na mifumo mipya iliyowekwa kiwandani hapo ambapo walitakiwa kulipwa tarehe 15 na badala yake walilipwa tarehe 17.

Wakulima hao wamesisitiza kwamba hakuna athari zozote zilizowapata kufuatia uamuzi wa serikali kutoa vibali vya kuagiza sukari nje kupunguza ongozeko la bei ya bidhaa hiyo ili kuleta ahueni kwa wananchi.

Vilevile wakulima hao wamesema kuwa vyama vyao vina ushirikiano mzuri na kiwanda cha sukari Kilombero na wanayo matumaini makubwa ya mageuzi ya zao hilo, kwa kuwa kiwanda hicho kinalenga kufanya upanuzi mkubwa utakaopelekea wakulima kuuza miwa kwa wingi zaidi.

Pia soma
Wakulima wa miwa kesho USO KWA USO na muheshimiwa Rais kwenye uzinduzi wa kiwanda cha sukari
 
Uhuni umezidi hii nchi jana tu nimezungumza na mtu yuko huko ni kilio tu maana kiwanda hakipokei miwa maana sukari yao imejaa kwenye maghala haitoki inayouzwa sokoni ni ile imejaa kwenye magodown ya wauza simu walio agiza kwa msamaha wa kodi bei ya jumla inakuwa rahisi ile reja reja iko pale pale.
 
Acha uongo, malori ya miwa yanaingia na kutoka viwandani usiku kucha, mchana kutwa, wewe habari zako za kuambiwa na mtu, inawezekana anayekwambia pengine yuko Mtwara au Kigoma
 
Back
Top Bottom