Wakristo: Vita ya Israel inayoendelea ni ishara tosha kuwa wakati wa kuja kwake mwana wa Adamu (YESU) umekaribia. Tuamke

Mtu Alie Nyikani

JF-Expert Member
Nov 9, 2022
781
1,747
Kutoka mitandaoni...

TAIFA LA ISRAEL NA UNABII WA SIKU ZA MWISHO.

Na Joshua Ntagala
Taifa la israel ni taifa takatifu la Mungu,
utakatifu wake sio katika matendo ya kiuungu lakini ni takatifu kwa maana ya kwamba limetengwa kwa ajili ya matumizi ya Mungu(ardhi yake,watu wake, wametengwa kwa ajili ya kutimiza mipamgo ya Mungu).

Wakati wa mfalme Sulemani Mungu alimwelekeza mfalme huyo ajenge hekalu na alimpa maelekezo ya kila hatua na namna ya kulijenga hekalu hilo.

Moja kati ya maelekezo hayo ni kuchinja NG"OMBE MKE MWEKUNDU,asiyekua na kipaku(doa) na kumchoma na majivu yake kuyatunza ili kutengeneza maji yanayoitwa maji ya FARAKANO ambayo yatatumika kulitakasa eneo ambapo hekalu hilo litajengwa(Hesb19:2,5-9).

Katika biblia kwa nyakati tofauti kuna mahekalu matatu ya sulemani

Hekalu la kwanza ni hilo alilolijenga mfalme sulemani ambalo linazungumzwa katika (2 nyakt 29:12-19),,Hekalu hili lilijegwa miaka 1000 kabla ya kristo lakini lilikuja kubomolewa mwaka wa 507 kabla ya kristo katika vita iliyotokea nyakati hizo.

Hatimaye lilijengwa tena hekalu la pili baada ya hilo katika eneo hilohilo na kwa maelekezo yale yale.

kitabu cha Nehemia kinazungumzia jinsi jitihada za kulijenga hekalu hilo zilivyokua.

Hekalu hilo la pili ndilo lililokuwepo mpaka wakati wa Yesu na katika vitabu vya injili tunaposoma habari za hekalu basi ni hili hekalu la pili linalozungumzwa hapo(Luka 2:46).

UNABII
Sikumoja Yesu alifika karibu na mji wa Yerusalemu akauona mji akaulilia na kutoa unabii huu "Halitasalia jiwe juu ya jiwe".

Akiwa na maana kwamba maadui wa israel watawapiga na kuusambaratisha mji wote kiasi cha kubomoa majengo yote yaliyomo humo ikiwa ni pamoja na hekalu hilo la pili (Luka19: 41-44).

Miaka 70 baadaye Yesu akiwa ameshapaa yapata miaka 30 hivi, hekalu hilo lilibomolewa tena na mwaka wa 125 taifa la israel lilisambaratishwa na kutawanywa kwa kipindi kirefu sana. Na eneo hilo lilikuja kukaliwa na waarabu na taifa la israel likawa halipo kabisa kwenye ramani ya dunia.

Lakini kama ilivyo,, taifa la israel ni taifa takatifu la Mungu haliwezi kupotea au ardhi yake kuchukuliwa na mtu mwingine yeyote maana ni ardhi ya Mungu.

(Walawi 25:23) Neno kabisa kabisa kama lilivyotumika hapa linamaana : Hata wakija watu wengine katika ardhi hio haitakua yao kabisa.

Sasa hekalu la tatu linakuja kutajwa kua litakuwepo tena; na kwa maana hio litakuja kujengwa tena.
Hekalu la tatu sasa linakuja kutajwa katika (2thesoln 2 :1-4) ambapo mpinga kristo ataketi akijifanya kua kama Mungu

*(Ufunuo 11:1-2)
Eneo yalipokuwapo hayo mahekalu ( la 1 na la 2) ni katika mlima unaoitwa "moria" katika mlima huu ndipo Ibrahimu alipo mpeleka isaka kumchinja na badala yake Mungu akamwonesha mwanakondoo wa kumchinja

(Mwanzo 22:1-2)
Eneo hili linajulikana kwa jina "TAMPLE MOUNT" na kwa sasa upo msikiti mkubwa sana unaoitwa "al aqsa". Pia upo msikiti mwingine unaoitwa " The dom of the rock".

Msikiti wa al aqsa ni mahala pa 3 kwa utakatifu kwa wa islamu pakwanza pakiwa ni
1. Maka
2. Madina
3. al aqsa+ dom of the rock( inaoneaha ni jinsi gani eneo hilo kurudi mikononi mwa israel itakavyokua sio kazi rahisi,itapasa vita)

MKAKATI WA ISRAEL KURUDI KATIKA ARDHI YAO
Ilitabiriwa baadae israeli watarudi katika ardhi yao na baada ya kurudi itakapo timia miaka 70 watapewa milki ya ardhi yao
(Daniel 9:1-2)
(Yer29:10-11)

Maneno hayo yalitimia kama yalivyo
Mwaka 1948 waisrael walijikusanya kutoka pande zote za dunia na kurudi katika ardhi yao na ilipiganwa vita ya masaa machache sana takribani 6 tu nawaisrael kuchukua sehemu ya ardhi yao na mwaka huo 1948 ndipo lilitangazwa kuwapo taifa la israeli.

Miaka 70 baadae 1948+ 70= 2018
6/12/2017-- Rais Donald Trump alitangaza rasmi kuutambua mji wa yerusalemu kua makao makuu ya israel na mwaka 2018 alizindua ubalozi wa marekani mjini yerusalemu na unabii ukatimia kama ulivyo.

Dunia nzima tarehe 21/12/2017 ilikaa kikao cha umoja wa mataifa kumpinga Donald trump kwa uamzi huo ili litimie lile neno " THOUGH ALL NATIONS OF THE EARTH ARE GATHERED AGAINST JERUSALEM(Well translated in English)"(Zekaria12:1,3).

Siku hio ilipigwa kura na mataifa 128 wakailaani marekani na rais wake kwa uamzi huo na kuilaani israel pamoja na azimio hilo.

Katika Africa: Togo pekee ndio waliwasapoti israel.

Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi walikwepa kupiga kura

Inasikitisha Tanzania tulipiga kura kinyume cha israel na marekani).

Katika ulimwengu wa Roho nyakati hizi marekani atapingwa sana, Donald trump atapingwa sana na wewe unaweza kua miongoni mwa wanaompinga lakini leo umepata ufunuo huu usiwe miongoni mwa wanaompinga Trump kwa sababu Trump anaisupport Israel, ukimpinga/ kumlaani Trump una ilaani isarael na atakae ilaani israel atalaaniwa.

Sasa maandalizi ya kulijenga hekalu la 3 katika eneo hilo la al aqsa yanaendelea ,na vifaa vyote vinavyo hitajika katika ujenzi vimeshanunuliwa kwa msaada wa kanisa kote duniani na 10/9/2018 (jumatatu), lilitokea tukio la kushangaza tena kwani alizaliwa ng'ombe mke mwekundu asie na doa lolote kwa uchunguzi wa kina yaani DNA test .Hii inamaanisha ng"ombe huyo ni maalum kabisa kwa ajili ya kutengeneza maji ya farakano yatakayo tumika kulitakasa eneo ulipo msikiti huo wa al aqsa, kabla ya ujenzi wa hekalu la 3 kama tulivyoona katika maelekezo alopewa suleman wakati anajenga hekalu la Kwanza hesabu 19:1-9) 29/9/2019 msikiti wa al aqsa ulizuiliwa na jeshi la Israel na kuwazuia waislam wote kuingia kufanya ibada

Manaake nini? Itafikia Muda waislam watakosa uvumilivu wa kisiasa na kuamua kuingia vitani na kwa sababu ya vitendo hivyo vya israel,,na katika vita hio ndipo msikiti huo utavunjwa ili lijengwe hekalu la 3 ambalo kanisa likiwa tayari limekwisha kunyakuliwa mpinga kristo atafunuliwa na kuketi katika hekalu hilo akijifanya yeye kua ni Mungu.

2Thesoln 2: 1-12
Mstari wa 4: mpinga kristo hana budi kuinuka na kuketi katika hekalu

Mstari wa 6: linalo mzuia mpinga kristo kujulikana na kuinuka waziwazi ni kanisa (yaani watakao nyakuliwa) mpaka watakapo ondolewa,yaani watakapo nyakuliwa

mstari wa 7: lakini ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi, uasi umekithiri kuliko unavyoweza kufikiri,, ni kwa sababu tu upo Tanzania unaweza usijue uasi unaoendelea huko duniani kwa sasa, lakini kanisa linajitahidi kuuzuia huo uasi mpaka litakapo ondolewa (yaan litakapo nyakuliwa).

Mstari wa 8: baada ya kanisa kunyakuliwa ndipo atafunuliwa yule asi yaani mpinga kristo ili aketi katika hekalu la 3 litakalokua tayari limeshajengwa.

Kwahyo muda mfupi sana kabla ya kubomolewa msikiti huo tukio la unyakuo wa kanisa lapasa kua limeshafanyika ili kumpisha mpinga kristo afanye mambo yake kama ilivyo andikwa.

Kama tunavyofahamu,
SIKU WALA SAA ya kuja kwa mwana wa adamu hakuna aijuaye na Yesu ametuachia dalili tu zitakazoonesha kua hio siku i karibu.

Kumbuka hakuna ajuae kua vita itatokea lini na ni muda gani msikiti huo utabomolewa na nini kitakua chanzo kikuu cha vita hio baina ya palestina na israel.Sasa tunapoyaona hayo yakiendelea tunajua tupo mwishoni kwa kiasi gani, na kwa hivyo tujiweke tayari.

Tusizidiwe na ndege wa angani ambao wanajua majira ya kujiliwa kwao ( yeremia 8 :7).

Tunajua kutambua ishara za uso wa mbingu kwamba kutakua na dhoruba lakini ishara za siku za mwisho hatuwezi kuzitambua (mathayo 16:3).

Tuwe kama wana wa isakari watu wenye akili za kujua nyakati ili wajue ni lipi liwapasalo kutenda katika nyakati hizo (1 nyakati 12:32).

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE NENO HILI AMBALO ROHO AYAAMBIA MAKANISA


(Ufunuo 22:11--12~~Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu;na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu;na mwenye haki na azidi kufanya haki;na mtakatifu na azidi kutakaswa.Tazama naja upesi,na ujira wangu u pamoja nami,kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.) we

NB: SIYO WAKIRSTO TU HATA WALE AMBAO BADO HAWAJAMKULI YESU KUWA MWOKOZI WA MAISHA YAO BASI MDA BADO UPO, KUBALI KUMPOKEA YESU LEO AWE BWANA NA MWOKOZI WAKO.
Kumbuka Bado kitambo kidogo Mwana wa Adamu atakuja.

Ubarikiwe wewe uliesoma huu ujumbe. Natumaini umepata kitu.
 
ukristo unaoujua umetokea kwa warumi,

israeli watu wengi ni waislamu, wayahudi,

acheni kukurupuka....

waisraeli hata hawana hayo mawazo ya 'taifa teule'
Kwani mm nimesema Ukirsto umetoka kwa Israel.

Hakuna aliekurupuka huu ni ujumbe upokee, usipokee ni juu yako lakin ujumbe umekufikia.

Uwe na Jion njema
 
Kutoka mitandaoni...

TAIFA LA ISRAEL NA UNABII WA SIKU ZA MWISHO.

Na Joshua Ntagala
Taifa la israel ni taifa takatifu la Mungu,
utakatifu wake sio katika matendo ya kiuungu lakini ni takatifu kwa maana ya kwamba limetengwa kwa ajili ya matumizi ya Mungu(ardhi yake,watu wake, wametengwa kwa ajili ya kutimiza mipamgo ya Mungu...

wewe Mtu Alie Nyikani siku nyingine ukipandisha andiko kama hili ni-tag!

Zingatia.
 
Yesu Bado sana kuja. Maana Kuna watu hawajui NENO la KRISTO. MFANO wamang'ati
Umakondeni huko mtu Hana msikitini Wala kanisa hakuna. Hiyo ni case ya tz.

Achana na nchi kama CHINA watu wanaabudu masanamu. Kwa hiyo tenda wema nenda zako usitegemee kuwa Ile vita ndo itamleta Yesu
 
kwenye vita hii nimejifunza mengi wana, kumbe JIHAD huwa inachagua watu wa kuwaendea. jihad kwa myahudi ni ngumu manake wanajua watafyekwa kweli si mchezo. kwanini boko haram, al shabab au isis wasiende huko? maisha matamu wewe.
 
Yesu Bado sana kuja. Maana Kuna watu hawajui NENO la KRISTO. MFANO wamang'ati
Umakondeni huko mtu Hana msikitini Wala kanisa hakuna. Hiyo ni case ya tz.

Achana na nchi kama CHINA watu wanaabudu masanamu. Kwa hiyo tenda wema nenda zako usitegemee kuwa Ile vita ndo itamleta Yesu

unataka achelewe chelewe kuja eeeh!

ha ha haa

acha aje bana...maana yaliyoandikwa no kama yote yapo ubaoni!
 
Yesu Bado sana kuja. Maana Kuna watu hawajui NENO la KRISTO. MFANO wamang'ati
Umakondeni huko mtu Hana msikitini Wala kanisa hakuna. Hiyo ni case ya tz.

Achana na nchi kama CHINA watu wanaabudu masanamu. Kwa hiyo tenda wema nenda zako usitegemee kuwa Ile vita ndo itamleta Yesu
Leo Injili inahubiriwa maporini na vijijin Injili inafika wewe upo wapi Injili haikufikii.
Kingine tambua siyo lazima uhubiriwe kwa Mdomo hata kwa kusikiliza Radio ukasikia mahubiri tayari Injili iemekufikia
 
Back
Top Bottom