JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,753
- 6,577
Wasimamizi wa soka letu wako tayari kuzibeba hizi timu ili kuwafurahisha watu kuliko kutenda haki.
Kadri muda unavyosonga, ligi inayoitwa ya nne kwa ubora barani Afrika inazidi kuwa ligi ya vituko kiasi kwamba inakuwa aibu kuisifia mbele ya watu wenye akili.
Waamuzi wa mechi ya leo wamechezesha kwa maelekezo mpaka wao wenyewe wameona aibu kwa vituko walivyofanya.
Waamuzi hawafanyi makosa kwa bahati mbaya kama wengi wanavyodhani, bali wanatekeleza maelekezo waliyopewa.
Muda umefika wa kuvunjwa kwa Kamati ya Waamuzi Tanzania pamoja na waamuzi wote, kwani hawana mchango wala msaada wowote katika maendeleo ya soka la nchi yetu.
Shame on you Waamuzi!