Wakili Onesmo Olengurumwa ashinda kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
24,217
28,135
29 July 2024

Mahakama ya Rufaa Tanzania
Dar es Salaam,
Tanzania

Kesi ya Onesmo Olengurumo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Tanzania


View: https://m.youtube.com/watch?v=M89ro2AWtds

Mahakama ya Rufaa Tanzania yatengua hukumu ya Mahakama Kuu katika kesi ya msingi iliyofungiliwa Mahakama Kuu kupinga .....

IN THE COURT OF APPEAL OF TANZANIA
AT PAR ES SALAAM
(CORAM: MWARI3A. 3.A.. RUMANYIKA. J.A. And MLACHA. 3.A/>
CIVIL APPEAL NO. 165 OF 2021

ONESMO OLE NGURUMWA.......................... APPELLANT

VERSUS

THE HONOURABLE ATTORNEY GENERAL............ .RESPONDENT

(Appeal from the Decision of the High Court of Tanzania, Main
Registry at Dar es Salaam)
(Mlvambina. 3.}
dated the 21st day of October, 2020 in Miscellaneous Civil Cause No. 36 of 2019

JUDGMENT OF THE COURT
9th July & 29th July, 2024
MLACHA. J.A.:

This is an appeal against the decision of the High Court of Tanzania Main Registry (The High Court), made in Miscellaneous Civil Cause No. 36 of 2019. The appellant, Onesmo Ole Ngurumwa was the petitioner. The Honourable Attorney General was the respondent. The appellant was challenging the constitutionality of provisions of the Criminal Procedure Act, Cap 20 R. E. 2002 (now R. E. 2019) (the CPA), which provide for the requirement of conducting preliminary inquiry and committal proceedings
at the subordinate court before a case is tried by the High Court. The petition was dismissed at the preliminary stage hence the appeal.

Page 1

READ MORE : Source : Onesmo Ole Ngurumwa vs The Honourable Attorney General (Civil Appeal No. 165 of 2021) [2024] TZCA 651 (29 July 2024)

Toka maktaba :
Kesi ya msingi iliyokuwa Mahakama Kuu :


12 February 2024

Kesi iliyofunguliwa na Mwanaharakati wa haki za Binadamu, Wakili Onesmo Olengurumwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Rufaa Na. 165 ya mwaka 2021 kuhusu kupinga vifungu vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai vinavyoruhusu washtakiwa kushtakiwa kwenye mahakama za chini ambazo hazina mamlaka ya kusikiliza kesi hizo (committal Proceedings) imeahirishwa mpaka itakapopangiwa siku nyingine ya kusikilizwa.

Kesi hiyo iliyopangwa kusikilizwa leo February 12, 2024 katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania, jijini Dar es Salaam mbele ya jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufani Mhe. Jaji Sehel, Mhe. Jaji Kente, na Mhe. Jaji Masoud saa 3:00 asubuhi

Upande waleta rufaa baada ya kufika mahakamani wameomba ahirisho kutokana na Jaji mmoja kati ya jopo la majaji watatu wa mahakama ya Rufani (Mhe. Jaji Masoud) kuwa alikuwa katika sehemu ya majaji wa mahakama kuu walioshiriki katika kesi hiyo ambayo uamuzi wake umekatiwa rufaa kwenye mahakama ya rufani kabla hajateuliwa rasmi kuwa Jaji wa mahakama ya rufani.

Akifafanua kuhusu ombi hilo Wakili Paul Kisabo amesema kuwa taratibu za kimahakama zinamnyima nafasi Jaji huyo kushiriki tena kwenye uamuzi akiwa Jaji wa mahakama ya Rufani kama alikuwa sehemu ya majaji wa mahakama kuu waliosikiliza kesi hiyo.

Upande wa Jamhuri kupitia mawakili wake wamekubaliana na ombi hilo ambapo Mahakama itapanga siku nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kwa kulingana na ombi husika.

Itakumbukwa Rufaa hiyo inatokana na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam uliotolewa mwaka 2020 ambapo Mahakama kuu ilitupilia mbali kesi hiyo.

Vifungu vinavyolalamikiwa ni kifungu namba 178, 243, 244, 245, 246, 247, 248, 249, 250, 256, 257,258 na 259 vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Katika Mahakama Kuu Wakili Olengurumwa aliitaka mahakama itoe amri ya Kubatilisha vifungu hivyo vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai akidai vinakiuka Katiba na haki za binadamu kwa mfano haki ya kusikilizwa kwa usawa, usawa mbele ya sheria pamoja na haki nyingine ambazo zipo katika Ibara ya 13 (1) (2) na (6) (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
 
29 July 2024

Mahakama ya Rufaa Tanzania
Dar es Salaam,
Tanzania

Kesi ya Onesmo Olengurumo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Tanzania
Wanachoweza wanasheria wa serikali ni kunyoa style mbalimbali za ndevu na mustachi tu
 
Back
Top Bottom