Wakili Madeleka: Fremu zilizovamia Mikocheni B wahalifu watatakiwa kumlipa bilioni mbili kama fidia alifanyiwa uvamizi huo

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
463
1,132
Wakili Peter Madeleka ambaye ni mwanasheria wa Juanna Chifunda amesema uharibifu uliofanyika kwenye fremu za maduka Mikocheni B ni uvamizi na wahusika watawawajibisha kwa mujibu wa sheria na ikiwemo mteja wake kidai fidia isiyopungua Shilingi bilioni mbili (2,000,000,000).

Wakili Madeleka ameeleza kuwa mteja wake tayari ameshatoa taarifa kwa jeshi la polisi kwa ajili ya upelelezi ili kupata wahusika waliofanya uvamizi huo na wakati huu wanasubiri taratibu za kipolisi zikishaisha waanze kufanya tathmini za uharibifu kwa hatua zaidi.

“lakini pamoja na hatua hizo ambazo polisi watachukua nitakaa na mteja wangu Juanna Chifunda kuona tunaweza tukachukua hatua gani nyingine za ziada za kisheria ili kupata madai…kuna hasara tumeipata hapa tutachukua hatua ya kufungua kesi za madai ili kuweza kudai fidia na kwa hakika fidia itakuwa ni kubwa tu, siyo chini ya Shilingi bilioni mbili (2,000,000,000/=) nadhani kwa haraka haraka…ili waliofanya kitendo hiki na wale walio nyuma yao wawajibike kwa mujibu wa sheria” ameeleza Wakili Madeleka.

Your browser is not able to display this video.
 
WAkili huwa anatafuta kesi na matukio au matukio yana mtafuta?
Kesi ya madada poa aliimalizaje au nayo ataifanya kimadai na siyo kijinai?
 
Hii inaonesha kuwa watu hawana elimu kuhusu sheria za kawaida kabisa kama masuala kuhusu mikataba.

Pia ni dalili kuwa raia na hata maofisa wa serikali na waliopo katika mifumo ya haki jinai wanahitaji kuwa wanapewa nafasi katika media kutoa elimu kuhusu sheria za kawaida kabisa.

Pia ripoti za hukumu za mahakama hasa zile za Mahakama Kuu ziwe zinaripotiwa katika vyombo vya habari na waandishi waliobobea ktk kuripoti kesi zilizopo Mahakama Kuu, hii itasaidia jamii ku share uelewa wa kuishi kwa kufuata mifumo ya kisheria.

Ukitazama media za Kenya kubwa na ndogo radio, vituo vya TV, online, magazeti n.k huwa wanaripoti mienendo ya kesi na hukumu kwa kina hivyo kuongeza wananchi kufahamu kuwa kuna mahakama, sheria na katiba katika jamii ili kutatua migogoro, mikataba maana yake nini n.k

MWAI KIBAKI / ALI HASSAN MWINYI ROAD MIKOCHENI 'B' DAR ES SALAAM

View: https://m.youtube.com/watch?v=Y8tupjKOcFQ

Habari za ziada :
TOKA MAHAKAMANI

IN THE HIGH COURT OF TANZANIA
(LAND DIVISION)
AT DAR ES SALAAM
LAND CASE NO. 221 OF 2021

HILAL Z. MAFTAH............. 1stPLAINTIFF
ABDULMAJID Z. MAFTAH......2ndPLAINTIFF
UWESU Z. MAFTAH.........3rdPLAINTIFF
YAHYA Z. MAFTAH.........4thPLAINTIFF

VERSUS

IBRAHIM ZAKARIA MAFTAH (as administrator of the estate of the late
AISHA BILAL HAMIS...1st DEFENDANT
ZAKARIA MAFTAH...2nd DEFENDANT
SALAMA ALLI ULIZA.3rd DEFENDANT
KURINGE REAL ESTATE COMPANY LIMITED.....4th DEFENDANT

Date of last order: 19/5/2022
Date ofruling: 7/6/2022

RULING
A. MSAFIRI, J.

On 22nd day of November 2021, the above named plaintiffs instituted the present suit against the defendants jointly and severally for reliefs inter
alia for declaration that intention to sale or sale of the property situated at Plot No. 29 Mikocheni Medium Density, Kinondoni Municipality, Dar es Salaam ...

SOMA ZAIDI : Source :
Hilal Z. Maftah & 3 Others vs Ibrahim Zakaria Maftah (as Admimistrator of the Estate of the Late Aisha Bilal Hamis & 3 Others (Land Case 221 of 2021) [2022] TZHCLandD 438 (7 June 2022)
 
Hapo nimesikiliza kwa umakini sana huyo Kuringe naona kama ameingizwa mkenge kwa kuuziwa mali kinyemela bila ya wamiliki wote kuridhia halafu badala ya kutuliza kichwa jinsi gani ya kufanya ndio anazidi kujichanganya kuwatuma mabaunsa waende kuvunja maduka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…