Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 558
- 1,325
Wakili Peter Madeleka ambaye ni mwanasheria wa Juanna Chifunda amesema uharibifu uliofanyika kwenye fremu za maduka Mikocheni B ni uvamizi na wahusika watawawajibisha kwa mujibu wa sheria na ikiwemo mteja wake kidai fidia isiyopungua Shilingi bilioni mbili (2,000,000,000).
Wakili Madeleka ameeleza kuwa mteja wake tayari ameshatoa taarifa kwa jeshi la polisi kwa ajili ya upelelezi ili kupata wahusika waliofanya uvamizi huo na wakati huu wanasubiri taratibu za kipolisi zikishaisha waanze kufanya tathmini za uharibifu kwa hatua zaidi.
“lakini pamoja na hatua hizo ambazo polisi watachukua nitakaa na mteja wangu Juanna Chifunda kuona tunaweza tukachukua hatua gani nyingine za ziada za kisheria ili kupata madai…kuna hasara tumeipata hapa tutachukua hatua ya kufungua kesi za madai ili kuweza kudai fidia na kwa hakika fidia itakuwa ni kubwa tu, siyo chini ya Shilingi bilioni mbili (2,000,000,000/=) nadhani kwa haraka haraka…ili waliofanya kitendo hiki na wale walio nyuma yao wawajibike kwa mujibu wa sheria” ameeleza Wakili Madeleka.