Wakili Kitale apingwa kesi dhidi ya TLS, uamuzi Agosti 9

jjackline

Senior Member
Jul 25, 2024
109
271
Mvutano wa kisheria unaoendelea Kuibuka katika shauri lililofunguliwa na Wakili Steven kitale katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza baada ya mjibu maombi wa nne, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuwasilisha pingamizi likiwa na hoja mbili.

Wajibu maombi katika shauri hilo namba 17558/2024, lililoitwa manakamani leo Jumanne Julal 30, 2024 kwa ajili ya kusikilizwa ni Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Mkurugenzi Mtendaji wa TLS, Baraza la Uongozi la TLS na AG.

Katika shauri hilo, Kitale anahoji amuzi wa kupandishwa ada za wanachama wa TLS wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) kutoka Sh118,000 hadi Sh200,000.

Anadai anapoomba mihutasari ya vikao vilivyopitisha ongezeko hilo amekuwa akipigwa danadana jambo lilimkwamisha asitekeleze wajibu wake kwa wanachama

Chanzo : Mwananchi
 
Tls ni wapuuzi haiwezekani wanachana wanaongezeka kila siku alafu bado unapandisha ada za mawakili?

Kwa wateja wapi!!???

Wateja wenyewe ni wa kunyang'anyana huku mtaani
 
Hawa n KIBOKO YA WACHAWI WENGINE WAKUFWATILIA SANAAAAA

KATIKA.MAHOJIANO AMA MDAHALOO MZEE.MMOJA ALILAAN SANA ONGEZEKO HILI WAPIGA DILI A SEHEMU 200000 SHAME N THEM
 
Mvutano wa kisheria unaoendelea Kuibuka katika shauri lililofunguliwa na Wakili Steven kitale katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza baada ya mjibu maombi wa nne, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuwasilisha pingamizi likiwa na hoja mbili.

Wajibu maombi katika shauri hilo namba 17558/2024, lililoitwa manakamani leo Jumanne Julal 30, 2024 kwa ajili ya kusikilizwa ni Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Mkurugenzi Mtendaji wa TLS, Baraza la Uongozi la TLS na AG.

Katika shauri hilo, Kitale anahoji amuzi wa kupandishwa ada za wanachama wa TLS wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) kutoka Sh118,000 hadi Sh200,000.

Anadai anapoomba mihutasari ya vikao vilivyopitisha ongezeko hilo amekuwa akipigwa danadana jambo lilimkwamisha asitekeleze wajibu wake kwa wanachama

Chanzo : Mwananchi
Naona kiwango kikubwa kinawekwa ili kupunguza wapiga Kura , na wapiga Kura wengi ni ambao watakuwa wamepata "usaidizi"
 
Back
Top Bottom