Wakazi: Wasanii hawajitambui. Kujipendekeza na uchawa ndio njia yao ya maokoto

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
746
2,093
Wakazi 1.jpg

Wakazi ameandika hivi kweye ukurasa wake wa Instagram:

Nimeona watu kwenye Twitter wakichukizwa na wasanii kwa kutosimama na jamii kupigania mambo muhimu, na mnafikiria kuanza kususia bidhaa zao (unsubscribe, unfollow, stop streaming, n.k.). Roma alitoa kauli ambayo hamjaielewa vizuri, na Nay Wa Mitego pia alitoa kauli. But I will put things in perspective.

Wasanii hawajitambui. Sababu ya zamani ya kuimba ilikuwa "misosi, mitungi na pamba," kisha ikaja fame, na sasa wanataka kuwa matajiri; specifically wanataka kuwa kama "Diamond." Sasa unadhani kuna atakayekumbuka wajibu wake kisanii kama kioo cha jamii?

Pili, hata mambo yao yanayowahusu hawazingatii; sasa unaanzaje kumtegemea kwenye mambo mengine? Katika vyama vya wasanii hawajiungi, na ukiwataka waanzishe Cooperative Union ya kulinda na kutetea maslahi yao huwaoni. International Conference za ACCES zimefanyika Dar kwa miaka miwili mfululizo, lakini mahudhurio hafifu (na ni sehemu muhimu ya kujifunza biashara ya muziki). Boomplay na Ziiki Media wamefanya workshops, lakini watu hawatokei. Unaanzaje kumtegemea mtu huyo?

Wasanii hawana hela; wengi hawaingizi kabisa, na wachache wanaoingiza wana matumizi ya juu na wamefungwa kwenye mikataba mibovu. So kujipendekeza na uchawa ndio njia yao ya maokoto. Unatarajia aache kumsifia Spika au Katibu Mkuu wa Wizara ili aje kupigania agenda za "choka mbaya" wenzao? Harmonize hana hata chorus au mstari wa kusifia wazazi wake kwa kumlea, lakini katoa album nzima kuhusu Mama Samia. Wakati angeweza kuimba kumwambia Rais shida zetu, pengine mambo yangebadilika.

Sikio la kufa, halisikii dawa!

Lakini, upande wa pili, kwa nini badala ya kususia hao wasio upande wenu, msiwainue wale ambao wapo nanyi? Nash MC juzi alikuwa na initiative ya kuleta awareness juu ya mambo yanayoendelea, lakini amelazimika kusitisha sababu ya ukosefu wa fedha za logistics.

Miradi yao mnai-support? Tusilalamike tu kwamba wasanii hawajafanya kitu na hawapo upande wetu, wakati na wao wanaona nyinyi pia hamuwaungi mkono.

Wasanii wakijitambua, wanaweza kuwa sehemu muhimu sana ya mapambano ya mabadiliko. Lakini itakuwa ngumu kama tutawandekeza njaa. Do your part, recognize your kind/tribe, and support them, lakini ku-boycott wasiojitambua ni kupoteza muda na focus!

Soma pia: Nay wa Mitego: Asilimia kubwa ya wasanii ni wa Serikali. Tuache uoga wa kukemea mambo ya kikatili na kutegemea Wasanii kupaza sauti
 
Wasaniii ni chawa, walimu ni chawa,polisi ni chawa,mahakama ni chawa,majaji ni chawa NK
 
Mwanangu Nash mc

Wasanii wengi tz tktk tu

Nashangaa mnao wasupport lazi zao

Ova
 
"ENJANGA ZA AMAYAGA" HAZIWEZI KUWA NA AKILI KICHWANI
 
Back
Top Bottom