uran
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 10,295
- 15,716
Wakuu,
Tuliambiwa jamaa wa NSSF wakimaliza kukusanya pesa yao, tutapita darajani bila malipo!
Mpaka sasa Miaka 6 inakaribia kuisha (lilizinduliwa 2016) hawa jamaa wanakusanya tu pesa.
Inamaana bado haijatimia? Tsh 4000 kwa siku na gharama za mafuta zilivyojuu, hawa watu wanatuonaje?
Tunaitaka Mamlaka ya NSSF wajitokeze waseme mpaka sasa wamekusanya Tsh ngapi na waweke wazi kilichobaki, hii ni kero sana.
Ni tabu tupu tukipita kwenye Kivuko nako ni Majanga! Kila siku tabu!! Mara tutoke kwa reverse mara Kivuko kihame njia Mara kishindwe kupaki!!
Watuambie kitu kimoja sasa.
Wasichukulie ukimya wetu kama Kigezo cha kuendelea kutubamiza.
=====
UPDATES;
======
Nimepata hii Taarifa Japo sijui kama ni ya kweli...
Pia, soma;
TAARIFA KWA UMMA
Salamu Wana Kigamboni,
Kutokana na kilio cha muda mrefu cha wana Kigamboni, Serikali imefanya mapitio ya tozo za daraja na kuzipunguza.
Serikali pia imekuja na utaratibu mpya ambayo wana Kigamboni walikuwa wanautaka kwa muda mrefu. Kuanzia sasa kutakuwa na tozo za safari moja, siku, wiki na mwezi.
Mfano: Atayelipia tozo ya siku ya siku ataweza kuvuka kwa idadi yoyote ya safari ndani ya siku husika.
Tozo mpya zimeanza kutumika kuanzia tarehe 20 Mei 2022.
NB: Nauli za wiki na mwezi zitachelewa kuanza kutokana na kazi inayoendelea ya kurekebisha mifumo.
Kuanzia sasa baadhi ya tozo zitakuwa kama ifuatavyo:
BODABODA
Bei itakuwa Tsh 300 kwa tripu, Tsh 500 kwa siku, Tsh 2000 kwa wiki na Tsh 5000 kwa mwezi.
*BAJAJ
Tsh 500 kwa tripu, Tsh 3000 kwa siku, Tsh 10,000 kwa wiki na Tsh 20,000.
MAGARI MADOGO
Tsh 1500 kwa tripu, Tsh 2500, Tsh 12,000 kwa Wiki na Tsh 35,000 kwa mwezi.
Kipekee namshukuru sana Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusikia kilio cha wana Kigamboni na kuagiza suala hili kufanyiwa kazi.
Nawashukuru Mawaziri Waheshimiwa Makame Mbarawa (Mb) na Prof Joyce Ndalichako (Mb) kwa usikivu na ushirikiano wao.
Pia, nawashukuru sana Makatibu Wakuu Eng Aisha Amour na Prof Jamal Katundu kwa kulibeba jambo hili kwa uzito unaostahili na kulifanyia kazi.
Aidha, namshukuru pia Mtendaji Mkuu wa NSSF Ndugu Masha Mshomba na Manejimenti yake kwa ushirikiano wao.
Wakati tunapongeza hatua hii ya awali ilichokuliwa na Serikali, kilio cha Wana Kigamboni ni KUONDOLEWA kabisa kwa tozo za Daraja la Nyerere
Natumai Serikali itaendelea kulifanyia kazi suala hili na hatimaye kuondoa kabisa tozo za Daraja la Nyerere.
Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Kigamboni
22.05.2022

Dar: Tozo za Daraja la Nyerere Kigamboni zimeshuka
Rais Samia Suluhu na Mbunge Faustine Ndugulile wamevunja kikwazo kigumu kabisa Cha maendeleo ya kigamboni. Sasa tozo zimeshuka na zitalipwa kwa siku badala Kila mtu anapovuka Hiki kilikuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya kigamboni. Kigamboni ikianza kujengwa itakuwa mji mzuri sana na...
www.jamiiforums.com