BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,811
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inatarajia kuanza ugawaji wa Vitambulisho (Kadi) kwa Wananchi waliojisajili na kupewa Namba za Utambulisho (NIN) katika Mikoa ya Dar na Mbeya hapo Desemba 12, 2023.
Taarifa iliyotolewa na NIDA imeeleza kuwa zoezi hilo litafanyika katika Ofisi za Serikali za Mitaa za Wilaya zote za Mikoa hiyo kwa kipindi cha siku 14 kuanzia tarehe tajwa.
Hatua ya NIDA inafuatia Mjadala uliofanywa na JamiiForums Septemba 7, 2023 ambapo Wananchi walihoji juu ya kusuasua kwa Utoaji Vitambulisho licha ya wengine kujiandikisha kwa zaidi ya miaka 5.